
Na Issa Mtuwa – Dodoma
Mafunzo ya Mkataba wa Utendaji
Kazi kwa Serikali na Taasisi za umma yameanza kufanyika kwa viongozi
waandamizi wa wizara ya Madini, wakuu wa idara na vitengo na maafisa
bajeti wa kila idara na kitengo kuhudhuria mafunzo hayo yanayotolewa na
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenye
ukumbi wa mikutano wa wizara ya madini
jijini Dodoma kuanzia leo tarehe 2
Desemba 2019.
Mafunzo hayo yanayotolewa kwa
wizara zote na tasisi za umma kwa awamu yanalenga kuziwezesha Taasisi za
Serikali kuandaa na kutekeleza mikataba ya utendaji kazi serikalini
tofauti na ule mkataba wa upimaji wa utekelezaji majukumu kwa watumishi
wa umma (OPRAS)
“Mikataba hii ni kwa mujibu wa
Waraka Na. 1 wa Mkuu wa Utumishi wa Umma wa mwaka 2018, pamoja na mambo
mengine unatoa maelekezo kwa wizara, idara zinazojitegemea, taasisi,
mamlaka, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa, wakala wa
serikali na mashirika ya umma kuandaa na nakufanya utekelezaji wa
mikataba ya utendeji kazi kwa kufuata malengo, shabaha na viashiria
vitakavyo ainishwa mwazo wa mwaka” alisema Charles Nakembetwa Afisa
Takwimu Mkuu ambae ni mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Pamoja na mambo mengine
aliyobainisha kuhusu mkataba huo wa utendaji kazi, serikali na taasisi
za umma zitakuwa zinapimwa kwa vigenzo mbalimbali vya utendaji na kwamba
upimwaji huo utashindanishwa wizara kwa wizara, taasisi kwa taasisi,
mikoa kwa mikoa, mashirka kwa mishirika n.k na kupata mshindi wa
utendaji kazi kwa mwaka husika kwa kila kundi.
“Kutakuwa na siku maalum ya utoaji
tuzo (zawadi) kwa watakao tekeleza mkataba wa utendaji kazi vizuri kwa
kila kundi na kwamba kwa watakaoshindwa kutekeleza mkataba huo pia
watapewa muda kujirekebisha na baadhi kupewa adhabu kwa mujibu wa vigezo
vitakavyo ainishwa” Alisema Kamugisha Rufulenge ambae ni mwenzeshaji
mwenza.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa
mkataba huo, katika ngazi ya wizara mtendaji mkuu wa usimamizi wa
utayarishaji na usimamizi wa utekelezaji wake atakuwa Mkurugenzi wa Sera
na Mipango (DPP) atakae simamia masuala yote kuhusu mkataba huo.
Akiongea mara baada siku ya kwanza
ya mafunzo hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Edwini Igenge
amesema mafunzo hayo yanaongeza hamasa kwa watendaji kuongeza bidii
katika utendaji kazi na kwamba kwa upande wa Wizara ya Madini wako
teyari kwa ajili ya uandaji na utekelezaji wa mkataba huo wa utendaji
kazi.
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi amesema serikali
imefanya kazi kubwa kuboresha utumishi wa Umma na mifumo mbalimbali
ambayo inarahisisha utendaji kazi akitolea mfano mfumo wa malipo ya
mishahara ya wafanyakazi (Payroll control).
Washiriki wa mafunzo hayo
hawakukosa kujadili kuhusu masuala ya mishahara ya watumishi wakijadili
katika sura tofauti tofauti hoja zikielekezwa kwa wawezeshaji huku
mengine yakitolewa ufafanuzi mengine wawezeshaji wakiahidi kuyachukuwa
na kuyapeleka mbele kwa hatua zaidi.
Mhsabu Mkuu wa Wizara ya Madini Anthony Tarimo alitaka kufahamu kuna hatuagani iliyofikiwa katika kufanya harmonization
ya mishahara kwa watumishi wa kada zote kama ambavyo iliwahi jadiliwa
kwa nyakati tofauti tofauti huku Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu
Kabigi Nsajigwa akizungumzia mitazamo na mijadala inayozungumzia kuhusu
upunguzwaji wa mishahara hasa kwa watumishi wa mashirika, taasisi,
mamlaka n.k. Amesema kimsingi kuna haja ya kutazamwa mtanzamo huo kama
ambavyo fikra za wengi wakitaka wenye mishahara mikubwa wapunguziwe
Ameongeza kuwa kitendo cha kuwapunguzia mishahara watu inaweza kuleta
ufanisi hafifu kwani maamuzi hayo yanapaswa kuzingatia mambo mengi kabla
ya uwamuzi huo huku akitolea mfano hapo nyuma ilivyowahi kupunguza
mishahara kwa watumishi wa kada ya uhasibu kwenye baadhi ya maeneo.
Mafunzo hayo ya siku tano
yaliyoanza leo yamehudhuriwa viongozi waandamizi wa WIzara ya Madini
akiwemo Kaimu Katibu Mkuu Edwini Igenge, Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu Issa Nchasi, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine
Olal, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani Mathias Abisai, Mwasibu Mkuu
Anthony Tarimo, Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi Ashura Urassa na Wakuu wote
wa Idara na Vitengo, Wakurugenzi Wasaidizi, Makamishna Wasaidizi na
Maafisa Bajeti wa kila idara na vitengo.
No comments :
Post a Comment