Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban,
(katikati), akiimba wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Kongamano la Kumi
la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) lililofanyika Dodoma. Wengine
kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi (STAMICO), Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Godfrey Mbanyi, Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Frederick Mwakibinga, na Mwakilishi kutoka Kenya Bw. Peter Momanyi.
Kamishana wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Frederick Mwakibinga,
akitoa taarifa fupi ya maadhimio yaliyopitishwa kwa ajili ya
utekelezaji kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi.
Amina Shaaban, ambae ni mgeni rasmi kabla ya kufunga Kongamano la Kumi la Waatalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC – Dodoma.
Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban, akizungumza wakati
akifunga Kongamano la Kumi la Waatalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB),
ambapo amewataka wataalamu hao kuzingatia miiko na maadili ya fani ya Ununuzi na Ugavi kama sheria inavyosema, Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban, akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfrey
Mbanyi, wakati wa kufunga Kongamano la Kumi la Waatalamu wa Ununuzi na
Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC – Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Kumi la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPSTB), wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban, (hayupo pichani), wakati akifunga Kongamano la Kumi la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma.
Meza Kuu
ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina
Shaaban, (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka
Zanzibar, wakati wa kufunga Kongamano la Kumi la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma.
(PICHA: JOSEPHINE MAJURA WFM – DODOMA).
……………………
Na: Peter Haule na Josephine Majura – WFM Dodoma
Serikali
imesema kuwa haitamvumilia mwanataaluma ya Ununuzi na Ugavi
atakayesababisha
upotevu wa rasilimali za nchi kwa kutozingatia kanuni
na sheria.
Hayo yamesemwa
Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi.
Amina Shaaban, alipokuwa akifunga Kongamano la 10 la Wataalamu wa
Ununuzi na Ugavi (PSPTB) zaidi ya 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Bi. Amina
Shaaban alisema kuwa fani ya Ununuzi na Ugavi ni adhimu na inalojukumu
kubwa katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa kati uliojikita
katika Viwanda ambapo fani hiyo ni muhimu upatikanaji wa bidhaa na
huduma.
“Yeyote
atakayepata nafasi ya kiutendaji, anapaswa kuzingatia miiko na maadili
ya fani ya ununuzi na ugavi kama anavyoongozwa na sheria katika kusukuma
juhudi za maendeleo. Atakaye kwamisha juhudi za Serikali katika kukuza
uchumi wa viwanda na kutoa huduma bora kwa wananchi asifumbiwe macho
wala kuhurumiwa”, alisema Bi. Amina Shaaban.
Alisema kuwa
anafurahishwa na hatua ya Bodi ya PSPTB ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa
Ununuzi na Ugavi ili waweze kushiriki kikamilifu katika hatua
mbalimbali za kukuza uchumi wa viwanda.
Amewataka
wataalamu wote waliohudhuria katika Kongamano hilo, kutekeleza maazimio
yote waliyokubaliana nayo na kufanya tathimini ya kiutendaji.
Kwa upande wake
Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Fredrick Mwakimbinga
alisema kuwa washiriki wamejadili mada mbalimbali na kuelekezana kuhusu
umuhimu wa fani hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda na pia
wamekumbushwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi, uzalendo na
kufuata sheria.
No comments :
Post a Comment