Afisa wa Wizara akiwa ndanii ya
Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea
Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji
Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika
viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Wizara wakiwa ndani ya

………………
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashiriki katika Maonesho ya
Nne ya
Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TANTRADE).
Kupitia Maonesho hayo, Wananchi
wanaelimishwa kuhusu majukumu ya Wizara na utekele zaji wake na namna
wizara na balozi za Tanzania zinavyofanya kazi ya kuvutia watalii na
wawekezaji kuja nchini kutembelea vivutio vya kitalii na kuwekeza
nchini.
Maonesho hayo ni utekelezaji kwa
vitendo kwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa
Viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2021.
Kauli mbiu ya maonesho hayo ya Tanzania sasa Tunajenga Viwanda inalenga kujenga na kuimarisha utamaduni wa Watanzania kutambua, kununua na kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini.
Maonyesho ya Nne ya Viwanda
yanahusisha wadau wa Sekta ya Viwanda na yataonesha fursa zilizopo
katika katika sekta ya viwanda na yatatoa fursa kwa wadau kuzungumza na
kujadili namna ya kujenga mahusiano endelevu ya biashara.
Maonyesho hayo pia yatawezesha kufanyika kwa mikutano ya wafanyabiashara ambayo itawakutanisha wauzaji na wanunuzi .
No comments :
Post a Comment