Mshindi wa jumla wa mashindano ya
gofu ya Tanzania Open 2019 Victor Joseph kutoka klabu ya Gymkhana mara
baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mh
Dumbaro katika mashindano yaliyomlizika katika Uwanja wa Kili Jijini
Arusha jana.

Mshindi wa Mikwaju ya jumla wa
mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019 M Chadha kutoka klabu ya Kili
mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi kutoka kampuni ya
Oryx Energy Sira Muhele katika mashindano yaliyomlizika katika Uwanja wa
Kili Jijini Arusha jana.
……………………..
Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Damas Ndumbaro
amehitimisha Mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania Open jijini Arusha
huku mcheza gofu
Victor Joseph kutoka klabu ya Gymkhana ya Dar es
Salaam akitwaa ubingwa wa mashindano hayo
Mchezaji huyo
kutoka Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana alifanikiwa kubakiza kombe
baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji
toka Nchi Sita kwa kupata Mikwaju (Gross) 294.
Siku ya
kwanza Mchezaji huyo alicheza 75,74,71 na 74 akifuatiwa Joseph Chinywai
kutoka Uganda aliyepata mikwaju 308 na kuwashinda wachezaji wengine
wa divisheni A walioshiriki mashindano hayo.
Katika
Mikwaju ya jumla Net Manraj Chadha wa kili golf aliibuka na Ushindi
baada ya kupata Mikwaju ya Jumla 291 huku akiwa amecheza 72,74,71 na 74
katika mzunguko wa Mwisho.
Mshindi
katika Divisheni B ni Joe Lee ambaye alipata mikwaju ya jumla 149 baada
ya kucheza 71 na 78 katika mzunguko wa pili huku kiwango chake cha
makosa kikiwa ni 18.
Mshindi
katika kundi la senior ni Boniface Nyiti wa Lugalo aliyepiga Mikwaju
yaa Jumla 162 baada yaa mzunguko wa kwanza kupata mikwaju 81 sawa na
mzunguko wa pili huku kiwango cha makosa kikiwa ni Nane.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TGU Criss Martin alisema
mashindano haya ni mashindano ya 69 tangu kuanzishwa kwake lakini
kumekuwa na Changamoto nyingi na kuomba Rais Magufuli kutupia Jicho
mchezo huo.
“ tunatambua
kazi kubwa ya Mh Rais katika Majukumu mbalimbali ambayo amekuwa akifanya
lakini tunaomba atupie jicho pia Mchezo huu umekuwa na mafanikio”
Alisema Mwenyekiti.
Kwa upande
wake Naibu Waziri Ndumbaro aliahidi kufikisha kilio chao kwa wahusika
ili kuendeleza mchezo huu nap engine kwa kuanzia ngazi yaa Mashuleni ili
kupata vipaji na kuzalisha wachezaji bora wakiwemo wa kulipwa
“ Nitafikisha
Kilio chenu Serikali ili kuboresha Mchezo huu lakini pia hakikisheni
mnasajili viwanja ili viwango vya Uchezaji viweze kutambulika Kimataifa
“. Alisema Naibu Waziri Ndumbalo
Aidha alisema
Mashindano yamefanikiwa na hiyo ni kutokana na Kazi nzuri waliyofanya
kwa kushirikiana na na kamati ,waratibu Verge Africa na wadhamini ambaao
wamefanya Zawadi kuwa Bora hivyo inahitaji kuendelezwa.
Klabu za
Tanzania zilzoshiriki mashindano haya yaliyodhaminiwa na Oryx, Super
Doll, Garda word, Coca Cola, Tanfoam, Hal na Serengeti ni Lugalo, Dar es
Salaam Gymkhana zote za Dar es Salaam, Morogoro Gymkhana, Arusha
Gymkhana, TPC, Moshi na Zanzibar Sea Cliff .
No comments :
Post a Comment