Viongozi wa idara ya
uhamiaji kutoka mkoani Arusha na jijini Dar es Salaam wakisikiliza maoni
kutoka kwa washiriki wa mkutano wa idara ya uhamiaji na wadau wa huduma
za kiuhamiaji mkoa wa Arusha uliofanyika jijini Arusha leo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakisikiliza maoni mbalimbali .
…………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Jumla ya wahamiaji
haramu 425 wamekamatwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Arusha katika
kipindi cha mwaka mmoja kuanzia januari hadi desemba mwaka huu.
Akiongea kwenye mkutano wa idara ya uhamiaji na wadau wa huduma za kiuhamiaji mkoa wa Arusha ,Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Arusha
,Abdallah Towo
amesema kuwa,wahamiaji hao haramu wamekamatwa kutoka nchi mbalimbali na
Kati yao 69 wamefikishwa mahakamani ,huku 66 wakifukuzwa nchini na
wengine 17 wakifungwa.
Amesema kuwa,ofisi ya
uhamiaji mkoa wa Arusha imeitisha mkutano wa wadau wa huduma za
uhamiaji kwa lengo la kupokea maoni na kutafuta suluhisho la kudumu
kuhusu changamoto mbalimbali za kiuhamiaji mkoani hapa.
Towo amefafanua
kuwa,katika kipindi cha Januari 2019 hadi novemba idara ya uhamiaji
imepokea pasipoti za kieletroniki 6,231 na shahada za dharura za
kusafiria 29,472 kwa watanzania waliohitaji kusafiri nje ya nchi.
Aidha katika sekta ya
utalii kwa kipindi hicho idara ya uhamiaji mkoa wa Arusha imetoa Viza
na pasipoti 1,402 kwa wageni walioingia nchini kwa madhumuni mbalimbali
ya utalii.
Amesema kuwa,katika
mpaka wa Namanga Raia wa Tanzania na wageni kutoka nchi mbalimbali
wapatao 124,106 wamewezeshwa kuingia nchini na ambapo Raia na wageni
125,681 wamewezeshwa kutoka nchini.
Amesema kuwa,kwa
upande wa wawekezaji idara hiyo imetoa jumla ya vibali vya ukazi 517
kwa wageni waliiongia nchini kwa madhumuni ya kuwekeza katika sekta ya
madini ,viwanda na biashara.
“katika kuhakikisha
kuwa mkoa wa Arusha upo salama idara ya uhamiaji imeimarisha udhibiti wa
wahamiaji haramu kwa kufanya kazi misako na Doria kwenye maeneo
mbalimbali ya mkoa huu na kwa kufanya hivi tumeweza kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa Sana.”amesema Towo.
Akiongea kwa niaba ya
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia
Muhongo amewataka watendaji wa idara ya uhamiaji kuzingatia maadili na
miongozo iliyopo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ili kuweza
kutatua changamoto zinazokabiliwa na idara hiyo.
Naye Afisa uhamiaji
mkoa wa Kilimanjaro,Tunu Ng’ondya amesema kuwa, changamoto ya wahamiaji
haramu iliyopo katika maeneo mbalimbali zinafanana ambapo kwa mkoa wa
Kilimanjaro wahamiaji haramu wamekuwa wakitoka Ethiopia kwenda nchi za
kusini.
Amesema kuwa,wamekuwa
wakishirikiana kwa pamoja na vikundi vya ulinzi na usalama chini ya
uongozi wao katika kuhakikisha kuwa mkoa huo unakuwa salama,huku
wakishirikiana na maafisa watendaji wa kata ambao wamekuwa makini kutoa
taarifa kwenye vyombo husika pindi wanapoona wageni katika maeneo yao.
No comments :
Post a Comment