
****************************************
Na Mwandishi wetuya
Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya
mchezo wa kuogelea ya Tanzania (The Tanzanite) imeshinda kombe la Shaba
katika mashindano ya Kanda ya Tatu Afrika yaliyomalizika jijini Nairobi,
Jumapili jioni.
Tanzania iliyowakilishwa na
waogeleaji 25 imemaliza katika nafasi ya tatu katika mashindano hayo
yaliyoshirikisha nchi tisa za Afrika kwa kukusanya jumla ya pointi 2,
044.50.
Wenyeji, Kenya ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 2, 447.50 na kufuatiwa na
Uganda iliyopata pointi 2, 392.
Mbali ya kushinda nafasi hiyo,
waogeleaji watatu wa Tanzania, Sydney Hardeman, Romeo Mihaly na Sylvia
Caloiaro walishinda vikombe kwa kushika nafasi ya kwanza kwa waogeleaji
wa wenye miaka yao.
Sydney alipata pointi 130 kwa
waogeleaji wenye miaka kati ya 11-12 wakati Romeo alikusanya pointi 118
katika umri huo huo na Sylvia alipata pointi 126.
Kwa mujibu wa matokeo hayo,
waogeleaji wa kike wa Tanzania waling’ara zaidi kwa kumaliza katika
nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 1,083 huku wenyeji, Kenya wakishika
nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 1,180 na Uganda katika nafasi ya
tatu kwa kupata pointi 851.
Kwa upande wa wanaume, Tanzania
ilikusanya pointi 865.5 na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Kenya
iliyomaliza ya pili kwa kupata pointi 1, 143.50 na Uganda iliyokuwa ya
kwanza kwa kupata pointi 1, 421.
Matokeo yanaonyesha kuwa Afrika
Kusini imeshika nafasi ya nne kwa kupata pointi 1, 540 wakati nafasi ya
tano imekwenda kwa Zambia kwa kupata pointi 1,386 na Burundi ya sita
kwa kupata pointi 866.
Waliokuwa mabingwa watetezi, Sudan
imeshindwa kufukuta baada ya kushika nafasi ya saba kwa kupata pointi
812 huku Djibouti ikipata pointi 105 na Malawi ikipata pointi 88.
Timu ya Tanzania iliundwa na
waoegeleaji Maria Bachmann, Sylvia Caloiaro, Kayla Temba, Sydney
Hardeman, Linnet Laiser, Sophia Latiff, Sarah Shariff, Avalon Fischer,
Nawal Shebe, Roos Nevelsteen, Eunike Mathayo na Lissa Stanley.
Wengine ni Mischa
Ngoashani, Augustino Lucas, Romeo Mihaly, Delhem Rashid, Terry Tarimo,
Aaron Akwenda, Singko Steiner, Ethan Alimanya, Sil Kleinveld, Ezra
Miller, Augustino Lucas, Ashraf Moez, Nathan Kagoro, na Peter Itatiro.
Meneja wa timu hiyo Hadija Shebe
aliwapongeza waogeleaji hao kwa matokeo hayo mazuri pamoja na changamoto
mbalimbali abazo zilisababisha baadhi ya waogeleaji kushindwa
kushiriki.
Hadija alisema kuwa walipanga kuwa
na waogeleaji 27, lakini waogeleaji wawili, Collins Saliboko anayesoma
nchini Uingereza na Hilal Hilal anayesoma Dubai wameshindwa kushiriki
kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.
“Matokeo yanaonyesha jinsi gani
Tanzania inafanya vyema katika mchezo huo na tunawaomba wadau watusaidie
kwani bila wafadhiri, mchezo hauwezi kufikia hatua ya juu kabisa ya
maendeleo,” alisema Hadija.
Caption:
Timu ya Taifa ya mchezo wa
kuogelea (The Tanzanite) wakiwa katika pozi baada ya kushinda nafasi ya
tatu katika mashindano ya Afrika ya Kanda ya Tatu yaliyomalizika
Jumapili mjini, Nairobi, Kenya.
No comments :
Post a Comment