
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
INAELEZWA kuwa kati ya wilaya zinazoongoza kwa
maambukizi makubwa ya VVU mkoani Pwani ni Kibaha Mjini ikifuatiwa na
Mkuranga na Chalinze.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Pwani,
katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi kimkoa ,huko Mwendapole ,Kibaha
Mji,katibu tawala wa mkoa ,Theresia Mmbando aliwataka wakuu wa wilaya
kushirikiana na wananchi kuweka mikakati na vipaombele ili kudhibiti
maambukizi mapya ya VVU.
Aidha ,alisema mkoa huo unakabiliwa na baadhi ya
changamoto zinazokwamisha juhudi za mapambano dhidi ya ugonjwa wa
ukimwi ikiwemo kukosekana kwa mashine ya kupima wingi wa virusi vya
Ukimwi ,biashara ya ngono,vigodoro na idadi ndogo ya vituo vya kutolea
huduma ya kufubaisha VVU.
Theresia alibainisha ,pia ipo changamoto ya mila
potofu katika jamii,ndoa za utotoni,maegesho ya malori,uzinzi,baadhi ya
wana ndoa kutokuwa waaminifu na watu wanaojidunga madawa ya kulevya.
Hata hivyo alisema,hadi kufikia 2017, takwimu za kiwango cha maambukizi ni 5.5.
Theresia alieleza licha ya hayo maambukizi mapya
ya virusi vya Ukimwi miongoni mwa wanaume,wanawake na vijana ,vijana
wenye umri kati ya miaka 15-49 ni mkubwa.
“Mwaka huu Januari -Oktoba maambukizi kwa
wanaume yalikuwa 2,944 kati ya wanaume 133,832 waliopima maambukizi ya
VVU sawa na asilimia 2.3.”
“Kwa wanawake yalikuwa ni 5,145 kati ya wanawake
187,222 waliopima maambukizi ya VVU sawa na asilimia 2.7 na kwa upande
wa vijana kuanzia miaka 15-24 maambukizi mapya ni 1,020 kati ya 95,559
waliopima sawa na asilimia 1.1″alieleza Theresia.
Nae mratibu wa
masuala ya Ukimwi ,Kibaha Mjini Siwema Cheru alisema ,halmashauri hiyo
inahamasisha jamii kuendelea kupata ushauri nasaha na kupima VVU na kwa
wale wanaogundulika na maambukizi ya VVU kupata ushauri na kuanzishiwa
dawa za kufubaza VVU .
Siwema alifafanua
,pia kuhamasisha WAVIU kujiunga kwenye vikundi ili kurahisisha utoaji
huduma na hadi sasa kuna vikundi 17 vya watu wanaoishi na Ukimwi na VVU.
Kwa upande wake
,makamu mwenyekiti wa KONGA ,Kibaha Mjini,Antonia Mango,aliomba kupitia
serikali za mitaa (TAMISEMI) itoe tamko kwenye halmashauri kutenga
asilimia fedha za shughuli za UKIMWI kama ilivyofanya kutenga asilimia
10 kwa ajili ya vikundi vya wanawake,vijana na walemavu.
No comments :
Post a Comment