Mkurugenzi wa huduma Mifugo
Tanzania kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga (Katikati)
Akizuzungumza wakati wa kufunga Mkutano huo, Kushoto ni Prof. Dominic
Kambarage Mwenyekiti wa TVA na Kulia ni Betha Dugange Afisa Mifugo
Mkuu,Idara ya ya Uratibu wa Sekta TAMISEMI aliyemuwakilishi wa
Mkurugenzi TAMISEMI.
Prof. Dominic Kambarage Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania TVA.

Washirki wa mkutano huo wakiwemo wanachama wa TVA na wadau wa Afya moja kutoka sekta mbalimbali.
…………………
Na: Calvin Edward Gwabara,Arusha
Serikali ya Tanzania imekipongeza
chama cha madaktari wa mifugo Tanzania TVA na wanachama wake kwa
jitihada mbalimbali inazozifanya katika kusaidia kuhakikisha sekta ya
mifugo inatoa mchango unaostahili kwa jamii na katika pato la Taifa.
Pongezi hizo zimetolewa na
Mkurugenzi wa huduma mifugo Tanzania kutoka wizara ya Mifugo na uvuvi
Prof. Hezron Nonga wakati akifunga mkutano wa mwaka wa TVA na kongamano
la kisayansi uliozungumzia dhana ya fya moja na kuwakutanisha wadau wa
mifugo,Kilimo,Mazingira,TAMISEMI,na Wizara ya afya lililofanyika kwenye
ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha IACC .
Prof. Nonga amesema tafiti
mbalimbali za kisayansi zilizowasilishwa kwenye mkutano huo zimesaidia
sana kujengeana uwezo miongoni mwao lakini pia kwa wadau wengine ambao
sio wataalamu wa mifugo lakini ni wadau wa dhana ya afya moja katika
kujua namna magonjwa hayo ya kuambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa
binadamu yanavyotokea na namna ya kuyadhibiti kwa pmoja wa ushirikiano.
” Tunasema mfano mchango wa sekta
ya mifugo upo chini ya asilimi 7.4 ya GDP bado hakuna tafiti
zilizofanywa kuonyesha mazao ya mifugo kama vile nyama,maziwa,mayai na
samaki vinachangia Protini Kiasi gani katika lishe ya binadamu hivyo ni
muhimu tafiti za aina hii pia zifanyike ili tujiridhishe mchango mdogo
wa sekta kama inavyosemwa” Alisema Mkurugenzi huyo wa huduma za mifugo
Tanzania Prof. Nonga
Prof. Nonga amesema Mkutano huo wa
kwanza wa dhana ya afya moja umesaidia kuwajengea uwezo wadau wa sekta
mbalimbali wanaunda dhana hiyo kupata uelewa wa pamoja na kuona umuhimu
wa ushirikiano huo katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali
ambazo zinahitaji ushirikiano wa sekta zaidia ya moja na hivyo kuisaidia
serikali katika kupanga mipango yake ya maendeleo katika kutimiza
agenda hiyo ya dunia.
Ameongeza kuwa sekta ya mifugo
inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo wadau hao kupitia TVA wameweza
kuzizungumzia kwa pamoja kama wataalamu wa Mifugo na kuweka mikakati ya
namna ya kuzitatua hali ambayo inasaidia utekelezaji wa majukumu ya
wizara ya mifugo baada ya kupata ushauri wa wataalamu hao waliobobea
kwenye sekta hiyo.
” Nawapongeza sana kwa majadiliano
mazuri mfano kwenye upande wa utoaji wa chanjo za mifugo, tunampango wa
kuzalisha chanjo nyingi sawa lakini bila kujua mbinu bora za utoaji na
usambazaji wa chanjo hizo tutajikuta tunakwama kama ambavyo tulikwama
kwenye utoaji wa chanjo ya homa ya mapafu ya ng’ombe lakini nyinyi
mmetushauri vyema kabisa kwenye mkuatano huu ushauri ambao serikali
tunakwenda kuufanyia kazi ili kuleta tija” Alisema Prof. Nonga.
Amesema kuwa Wizara ya kurugenzi
yake itahakikisha inasaidia mifugo ya nchi hii inakuwa salama na kustawi
inavyotakiwa na kutokuwa chanzo ya magonjwa yanayotoka kwa mifugo
kwenda kwa binadamu na hivyo kuwezesha nyama ya Tanzania kwenda nje ya
nchi kitu ambacho hakifanyiki kwa sasa kutokana na magonjwa mifugo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama cha Mdaktari wa Mifugo Tanzania TVA Prof. Dominic Kambarage
ameshukuru muitikio mzuri wa wadau wa afya moja kwenye mkutano huo
muhimu na wa kwanza nchini na kutumia fursa hiyo kuomba ushirikiano
zaidi katika utekelezaji wa dhana hiyo ya afya moja kwa sekta zote.
Prof. Kambarage ameomba viongozi
wa Wizara ya Mifugo na uvuvi,TAMISEMI,Utumishi kusikiliza changamoto za
wataalamu hao ambazo zinakwamisha utendaji wao ili waweze kufanya kazi
kwa moyo na hivyo kulisaidia taifa kupitia taaluma zao badala ya kufanya
kazi wakiwa na malalamiko mbalimbali yanayopunguza ari yao ya kazi.
Mwenyekiti huyo wa TVA amesema
mada mbalimbali za kisayansi zimewasilishwa kutoka kwa watafiti katika
sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo,Afya,Tasisi za elimu ya juu na taasisi
za utafiti ambazo zimesaidia kujenga uelewa wa pamoja juu ya changamoto
zinazoikabili sekta ya mifugoafya na mazingira na hivyo kuweka maazimio
ya namna ya kuzitatua kwa maslahi mapana ya wananchi na taifa.
No comments :
Post a Comment