
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi wa NSSF, Balozi Alli Siwa, wakati
alipokagua Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa na Shirika la
Nyumba la Taifa ya Ujenzi wa nyumba Tuangoma, Mtoni Kijichi na Dungu,
Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya
Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akioneshwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akikagua
mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni,
jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati
akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya
Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi, wakati alipotembelea mradi wa nyumba za NHC, zilizopo Mtoni
Kijichi katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27,
2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiwasalimia Watoto wa Chekechea wa Shule ya Kids Paradise, iliyopo
ndani ya Mradi wa Nyumba za NHC, Mtoni Kijichi wilayani Kigamboni,
jijini Dar es Salaam, wakati alipokagua Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii wa Taifa na Shirika la Nyumba la Taifa ya Ujenzi wa nyumba
Tuangoma, Mtoni Kijichi na Dungu, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua mradi wa nyumba za Watumishi Housing, uliyopo Dege wilayani
Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za Watumishi
Housing, uliyopo Dege wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba
27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
****************************************
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema nyumba zote zinazojengwa na Taasisi za Umma
katika wilaya Kigamboni jijini Dar es salaam zinapaswa kukamilika haraka
ili ziuzwe ua kupangishwa kama ilivyokusudiwa.
Ameyasema hayo
leo (Jumatano, Novemba 27, 2019) baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa
nyumba za NSSF, NHC na Watumishi Housing iliyopo katika wilaya ya
Kigamboni.
Waziri Mkuu
amesema inasikitisha kuona kwamba watumishi wa umma na wananchi jijini
Dar es Salaam hawana nyumba nzuri za kuishi wakati zipo nyumba
nyingi nzuri zimejengwa na zinahitahi umaliziaji mdogo tu ili ziweze
kukalika.
Hivyo, Waziri
Mkuu ameitaka Menejimenti ya NSSF kakamilisha haraka ujenzi na uwekaji
wa miundombinu ya umeme, maji safi na maji taka katika nyumba zake 161
zilizoko Tuangoma, 820 zilizoko Mtoni Kijichi na 439 zilizoko Dungu ili
ziuzwe na kuepusha uwezekano wa uharibifu unaoweza kutokea kwa nyumba
hizo kakaa muda mrefu bila kupata wanunuzi au wapangaji.
Ili kufanikisha
jambo hilo Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mthamini Mkuu wa Serikali
atathimini nyumba hizo na kutoa bei halisi ya soko kwa sasa ili
kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na
kupanga katika nyumba hizo.
Pia, Waziri
Mkuu amemtaka Mkuu wa wilaya na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya
Kigamboni kuwasaidia watumishi wa wilaya na Halmashauri hiyo kuingia
mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi hao kupewa kipaumbele katika
kununua au kupanga kwenye nyumba hizo.
Mheshimiwa
Majaliwa pia ameitaka Menejimenti ya NSSF kufikiria namna ya kuzungumza
na viongozi wa vyuo mabalimbali kama vile Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM), Chuo cha Mwalimu Nyerere ili wanafunzi wa vyuo hivyo wapatiwe
fursa ya kupanga katika nyumba hizo kwa bei watakazomudu.
Pia Mheshimiwa
Majaliwa ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam ukishirikiana na
SUMATRA kuanzisha njia za mabasi ya daladala zitakazoanzia au kupitia
kwenye nyumba za NSSF Mtoni Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na
wananchi watakaonunua nyumba hizo kupata usafiri wa umma.
Vilevile,
Waziri Mkuu ameuagiaza uongozi huo kuhakikisha kwamba eneo la Mtoni
Kijichi zilipojengwa nyumba za NSSF na NHC linapata huduma za Shule,
Kituo cha Afya na Kituo cha Polisi kwani litakuwa na wakazi wengi .
Ili kuongeza
thamani ya nyumba hizo na kuvutia wapangaji na wanunuzi, Mheshimiwa
Majaliwa ameitaka Menejimenti ya NSSF kuboresha barabara kwenye mitaa
yote zilipojengwa nyumba hizo kwa kushirikiana na TARURA.
“Nashauri
ziwekwe taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya nyumba hizi ili
kupendezesha eneo na kuwafanya wananchi wahamasike kununua na kuishi
katika nyumba hizi” amesema Majaliwa.
Akiwa kwenye
Mradi wa Nyumba za NHC Mtoni Kijichi, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea
Shule ya Awali ya Kids Paradise na kufurahishwa na utaratibu mzuri wa
shirika hilo wa kukumbuka kujenga jengo zuri la Shule hiyo na
kulipangisha ili kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi katika nyumba hizo
wanapata fursa ya kusoma elimu ya awali.
Akizungumza
baada ya kukagua Mradi wa ujenzi wa nyumba za NHC Mwongozo, Mheshimiwa
Majaliwa ameutaka uongozi wa NHC kuwa karibu na wateja wanaopanga au
kununua nyumba zao. “ Shughulikieni malalamiko yote yanayotolewa na
wateja wenu ili wajenge imani kwenu, Alisisitiza Majaliwa.
Waziri wa nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
Jenista Mhagama alisema wizara yake imeyapokea maelekezo yote
yaliyotolewa na Waziri Mkuu na kwamba watafanya kila njia ili
kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au
kupangishwa.
Naye Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, william Lukuvi alimwambia Waziri
Mkuu kuwa amekwishatoa maagizo kwa NHC ijenge uzio japo wa waya na
wapande michongoma ili kuweka ulizi kwenye eneo la nyumba zao za Dungu.
Mheshimiwa
Lukuvi alisema amewapa NHC miezi mitatu ili wafanye marekebisho katika
nyumba ambazo zimelalamikiwa na wateja kuwa zina kasoro ili kujenga
imani kwa wateja wao.
Mapemba
Mkadiriaji Majengo wa NSSF, Abon Mhando ambaye pia ni Kaimu Meneja
wa Miradi wa NSSF alimwambia Waziri Mkuu kuwa Mradi wa ujenzi wa nyumba
wa Tuangoma una jumla ya nyumba 161 na kati ya hizo nyumba 76
zimekamilika. Aliwataja wakandarasi wanaojenga mradi huo kuwa ni Kampuni
za CASCO, Advent na NANDRA.
Alisema Mradi
wa Dungu una jumla ya nyumba 439 na kati ya hizo nyumba 95 zimekamilika
na jumla ya makampuni 13 yameshiriki katika ujenzi wa mrdi huo.
Kuhsu mradi wa Mtooni Kijichi Mhando alisema mradi huo una jumla ya nyumba 820 na kati ya hizo nyumba 417 zimekamilika.
No comments :
Post a Comment