
*************************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
MBUNGE viti maalum mkoa wa Arusha,
Amina Mollel, ameiomba serikali kuboresha miundo mbinu kwenye shule za
msingi na sekondari ili kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye
ulemavu wa viungo waweze kupata maeneo salama ya kujisaidia kuliko hali
ilivyo sasa.
Mbunge huyo ametoa kilio hicho
Novemba 27 kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa,RCC, alipokuwa
akichangia hoja ya Idara ya afya iliyowasilishwa na mganga mkuu wa mkoa,
Dakta Wedson Sichelwe, iliyokuwa ikielezea hali ya patikanaji wa dawa
mkoani humo.
Mbunge, huyo alisema miundo mbinu
iliyopo kwenye shule hizo sio rafiki kwa wenye ulemavu ,ambapo kwenye
ziara yake aliyoifanya shule mbalimbali mkoani humo ameshuhudia walemavu
wakitaabika kwenda kwenye vyoo .
Alisema hali hiyo inauma kwa kuwa
walemavu wanataabika hivyo kutokana na serikali kutekeleza mpango wa
chakula bure unatakiwa uende sambamba na uboreshaji wa miundo mbinu
rafiki kwa walemavu .
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Monduli, Julius Kalanga, ameiomba serikali kuhakikisha dawa zinawafikia
wananchi na kuwaondolea usumbufu wa kupata dawa mara baada vipimo vya
magonjwa.
Alisema taarifa ya upatikanaji
iliyotolewa na mganga mkuu hailingani na hali halisi ilivyo vijijini
ingawa serikali inatoa fedha za dawa na halmashauri zinalipa
wazabuni.ambao wamekuwa hawafikishi huduma hizo kwa wananchhi.
Alisema kuna baadhi ya wazabuni
hawana uwezo hivyo waangaliwe upya utendaji wao kwa kuwa wanasababisha
usumbufu kwa wananchi kwa sababu hawana uwezo na kusababisha mlundikano
wa wananchi kusafiri umbali mrefu kusaka dawa.
Kwa upande wake Katibu tawala wa
wilaya ya Longido, Toba Nguvilo, alisema katika kata za Kitumbeine na
Girarungwe, wilayani Longido, Zahanati na vituo vya afya
vinavyomilikiwa na Kanisa la KKKT kadi za bima ya afya iliyoboreshwa
hazipokelewi.
Alisema wananchi wenye kadi za
bima iliyoboreshwa wamekuwa wakishindwa kupata huduma ya tiba kutokana
na kadi hizo kutokupokelewa wala kukubalika na hivyo kujikuta wakikosa
huduma za matibabu.
Kwa upande wake mchungaji Simon
Dereva wa KKKT kwa niaba ya askofu Simoni Masangwa, alisema
watalishughulikia tatizo ili kadi hizo ziweze kupokelewa na wananchi
wapate huduma huduma za matibabu kwa kuwa serikali imeonyesha
ushirikiano wa hali ya juu.
Awali akiwakilisha taarifa yake
mganga mkuu wa mkoa,Dakta Wedson Sichelwe, alisema kiwango cha
upatikanaji wa dawa katika mkoa huo ni asilimia 99% na kuwaondoa hofu
wajumbe na wananchi kuwa suala la dawa katika mkoa sio changamoto kama
ilivyokuwa siku za nyuma
Wakati huo huo imeelezwa kuwa
mkoa wa Arusha una upungufu wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari
262 ,ambapo wilaya ya Meru inaongoza kwa kuwa na upungufu wa vyumba 66
huku wilayua ya Longido ikiwa na upungufu wa vyumba vine tu.
Katibu tawala mkoa wa Arusha,
Richard Kwitega, ameyasema hayo alipokuwa akiwakilisha taarifa ya
utekelezaji war obo ya pili ya mwaka ya kamati ya ushauri mkoa ya mwaka
2018/19.
Alisema mkoa katika kutekeleza
maazimio ya kikao kilichopita cha mwezi Marchi mwaka huu mkoa unaanza
mkakati wa kujenga vyumba hivyo vya madarasa kwa shule za sekondari
ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi watakaojiunga na kidatoo cha kwanza
mwakani.
Kuhusu afya ,alisema
Kwitega,amesema kuwa mkoa unaendelea na ujenzi wa hospital za wilaya za
Longido, Karatu Ngorongoro na halmashauri ya Jiji la Arusha ,ambapo
ujenzi wake upo kwenye kiwango kizuri.
Alisema kikao kilichopita
msisitizo ulikuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo Sekretari
ya mkoa na mamlaka za serikali za mitaa mwaka 2018/19 mkoa
uliidhinishiwa shilingi ,67,570,830,394.10 kwa ajili ya miradi.
No comments :
Post a Comment