
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifungua Kongamano la 6
la mwaka la Afya lenye lengo la kuwaleta pamoja Wadau mbali mbali
katika Sekta ya Afya, ili kujadili maendeleo na changamoto ambazo nchi
inakabiliana nazo.


Wadau mbali mbali wa Sekta ya
Afya wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Kongamano la 6 la mwaka la Afya
lenye lengo la kuwaleta pamoja Wadau mbali mbali katika Sekta ya Afya,
kauli mbiu ya “ufanisi na matokeo ” katika utoaji huduma za Afya.

Wadau mbali mbali wa Sekta ya
Afya wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Kongamano la 6 la mwaka la
Afya lenye lengo la kuwaleta pamoja Wadau mbali mbali katika Sekta ya
Afya, ili kujadili maendeleo na changamoto ambazo nchi inakabiliana
nazo, lenye kauli mbiu ya “ufanisi na matokeo ” katika utoaji huduma za
Afya.

Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri waUmmy Mwalimu akiwa na Wadau wa masuala ya Afya kutoka Sekta
mbali mbali za Kiserikali na Binafsi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 6
la mwaka la Afya lenye kauli mbiu ya “ufanisi na matokeo ” katika
utoaji huduma za Afya.
………………………………………………..
Na Rayson Mwisemba, WAMJW- DOM
Sera Mpya ya Afya ya Mwaka 2019 –
2020 itajikita katika Kinga ili kukabiliana na mzigo wa gharama za
matibabu ambazo zinawatesa Wananchi katika ngazi ya Jamii na nchi kwa
ujumla.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu jiji hapa
wakati akifungua kongamano la 6 la mwaka la Afya lenye lengo la
kuwaleta pamoja Wadau mbali mbali katika Sekta ya Afya, ili kujadili
maendeleo na changamoto ambazo nchi inakabiliana nazo, lenye kauli mbiu
ya “ufanisi na matokeo ” katika utoaji huduma za Afya.
“Ukiangalia Sera ya Afya ya Mwaka
2007, tulijikita zaidi kwenye mambo ya Tiba, sio kinga, kwahiyo Sera
hii mpya ya Afya ya mwaka 2019 – 2020 itajiwekeza zaidi katika masuala
ya Kinga sio Tiba, kwa sababu wote tunaamini Kinga ni bora kuliko tiba”
alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo alisema Sera hiyo
inapendekeza kwamba, Serikali kwa kushirikiana na Wadau iweke
miundombinu ya kutoa huduma za Afya kwa kuzingatia vigezo vya jografia
ya eneo husika, idadi ya watu waliopo katika eneo, na kuangalia mzigo wa
magonjwa katika eneo hilo.
“Serikali kwa kushirikiana na
Wadau tutaweka miundombinu ya kutoa huduma za Afya kwa kuzingatia vigezo
vitatu, vigezo vya kijografia ya eneo husika, vigezo vya idadi ya watu
waliopo katika eneo, na vigezo cha tatu tutaangalia mzigo wa magonjwa
katika eneo hilo ili kumpatia mwananchi huduma stahiki na kwa wakati
kulingana na vigezo hivi” Alisema.
Aidha , amesema Sera hiyo mpya
inayotarajia kuanza kutumika mwaka huu wa fedha , Serikali itaendelea
kutambua mchango wa Sekta Binafsi katika utoaji wa huduma za Afya kwa
wananchi, jambo litalosaidia kupunguza mzigo wa utoaji huduma.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya
Kongamano la Afya Omary Nchili amesema kuwa, lengo la Mkutano huo, ni
kujadili changamoto na matokeo chanya katika Sekta ya Afya, ili kuongeza
ufanisi katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi.
“Tumekutana hapa Wadau mbali
mbali kuweza kujadili, changamoto pamoja na matokeo chanya katika Sekta
ya Afya, kwa ufanisi, hivyo tutakuwa hapa kwa siku mbili ambazo
tutapembua kwa undani kuhusu upatikanaji wa huduma kwa gharama ndogo na
upatikanaji wa huduma kwa ujumla ” alisema.
Kongamano hilo la siku mbili
limeandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Wizara ya Afya Zanzibar, Tume ya huduma ya Kijamii ya
Kikristo, Bakwata na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tindwa Medical
Services inayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete .
No comments :
Post a Comment