Saturday, November 30, 2019

BODI YA URATIBU WA NGOs YATAHADHARISHA MASHIRIKA KUFANYA SIASA



Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Richard Faustine Sambaiga (Mwenye koti) akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akifafanua jambo kwa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Mjumbe wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Zena Mabeyo akifafanua jambo wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Mwakilishi wa Shirika la The Kesho Fund Bw. Petro Okoth akifafanua jambo katika kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Mwakilishi wa Shirika la Foundation for Farmer’s Service Bi. Lydia Kamugisha akifafanua jambo katika kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Baadhi ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Mwanza wakisikiliza maelezo kutoka kwa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipotembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Richard Faustine Sambaiga (Mwenye koti) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Mwanza mara baada ya kikao kati ya Bodi hiyo na wadau hao.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
********************************
Na Mwandishi Wetu Mwanza
Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeyatahadharisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutojihususha na masuala ya kisiasa bali wasimamie Katiba zao katika
kutekeleza majukumu yao ya kuisadida jamii ya watanzania.
Mwenyekiti wa Bodi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Dkt. Richard Faustine Sambaiga ametoa tahadhari hiyo mkoani Mwanza alipokutana na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiseikali mara baaad ya kutembeea baadhi ya Mashiria hayo kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mashriika ya mkoa wa Mwanza.
Dkt. Sambaiga amesema kuwa katika kipindi cha uchaguzi wadau wengi wa NGOs wanahama katika majukumu yao na kuanza kupeperusha bendera za watu wengine na sio kuihudumia jamii inayowazunguka kama Katiba zao zinavyoelekeza.
Pia amewataka wadau wanaofanya kazi za kutoa elimu kwa wapiga kura kutumia fursa ya uchaguzi Mkuu ujao kuchangamkia fursa hiyo na kuwataka kutoa elimu ya kupiga kura na sio kampeni za kisiasa.
“Kama unaona unataka kujiingiza katika masuala ya kisiasa achana na kazi za NGOs simama wewe kama wewe na sio kuitumia NGO kwa ajili ya kufanya kampeni au kuwafanyia watu kampeni za kisiasa” alisema Dkt. Sambaiga
Dkt. Sambaiga ameyataka Mashirika kujiendesha kitaasisi na sio kuendesha Mashirika hayo kwa maslahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu bali watekeleze majukumu kwa mujibu wa Katiba yao waliosajili Shirika.
“Tumetembelea Shirika moja ofisi zipo nyumbani kwa Mkurugenzi tukaomba mikataba ya fedha hana sasa hili Shirika linaendeshwaje na mtu mmoja na lina wajumbe zaidi ya kumi”alisisitiza Dkt. Sambaiga
Kwa upande wake Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao amesema kuwa Ofisi yake imeamua kutembelea Mashirika mkoani Mwanza kufuatilia miradi ianyotekelezwa na Mashirka hayo kwa jamii.
“Tumekuja kwenu kwa lengo la kujionea miradi mnayoitekeleza katika jamii na kuona kwa uwazi na uwajibikaji wa Mashirika yenu kwa jamii ikiwemo Jamii husika  kujua miradi inayotekelewa na gharama zake” alisema Bi. Vickness.
Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi inayofanya na Mashirika yaliyopo mkoani Mwanza kwa lengo la kujiridhisha juu ya miradi hiyo na manufaa yake katika jamii.

No comments :

Post a Comment