Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka akizungumza wakati wa mkutano kati ya Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) na Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya biashara nje ya nchi (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi na Mshauri wa Masuala ya Mikakati wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Bi. Catherine Kimaryo akizungumza na Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya biashara nje ya nchi ulioandaliwa na Wizara
ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania (TANTRADE), (hawapo pichani), kulia ni Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin
Rutageruka Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka
Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka, (wa pili kushoto) na
Ujumbe kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), ukiongozwa na Mkurugenzi
wa Masuala ya Fedha Bw. Lloyd Muposhi (wa kwanza kushoto), wakiwa
katika picha ya pamaoja na Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya
biashara nje ya nchi, mkutano huo umefanyika Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya biashara nje ya nchi wakifuatilia kwa makini mazungumzo yalikuwa yakiendelea kati yao na Uongozi wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), walipokutana kwa ajili ya kuboresha biashara kati yao uliondaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Josephine Majura-Wizara ya Fedha)
************************************
Wafanyabiashara nchini kwa kuwapatia mikopo nafuu
itakayowawezesha kusafirisha na kuuza bidhaa za kilimo nje ya nchi
Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Bw. Lloyd Muposhi, wakati ujumbe wa Benki hiyo uliopo nchini kwa ziara ya kikazi, ulipokutana na kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara wanaojihusisha na uuzaji wa mazao hayo nje ya nchi ikiwemo nafaka, chai, kahawa na katani.
Bw. Muposhi,
ameeleza kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalikua mazuri yenye
kujenga ambapo kwa mwaka ujao wa fedha ameahidi benki hiyo itawawezesha
wafanyabishara ama sekta binafsi kimtaji ili waweze kukuza mitaji yao na
kufanya biashara ya ushindani na yenye tija.
Kwa upande wake Mkurenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin
Rutageruka ameishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuratibu mkutano
huo na kuwakutanisha Wafanyabiashara na Uongozi wa Benki ya Biashara na
Maendeleo ambapo wamepata muda wakubadilishana uzoefu na kujadili mambo
mbalimbali zikiwemo changamoto mbalimbali zinazokabili usafirishaji wa
bidhaa nje ya nchi, uzoefu wa kufanya biashara pamoja na ukosefu wa
mitaji.
Bw. Edwin
alisema changamoto kubwa iliyopo kwa Wafanyabiashara wa ndani ni ukosefu
wa mitaji kwa kuwa ni gharama kubwa kusafirisha bidhaa kwenda nje ya
nchi hivyo iwapo TDB wataanza kutoa ufadhili kwa Wafanyabiashara wa
Tanzania watakuwa wamewasaidia sana kuondokana na tatizo hilo.
Naye mmoja wa
Wafanyabiashara walioshiriki katika mkutano huo Mkurugenzi wa
ALASKATANZANIA, Bi. Jennifer Bash ameipongeza Serikali kwa kuandaa
mkutano huo kwani umetoa fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya
Wafanyabiashara hao na uongozi wa benki hiyo.
Alieleza kuwa
changamoto kubwa inayowakabili Wafanyabiashara wengi ni uhaba wa fedha
na mitaji hivyo mkutano huo umetoa mwanga kwao kwa kuwa wamezungumza
mambo mengi ambayo iwapo yatatekelezwa yatapunguza ombwe lililopo la
ufanisi wa biashara kwa wafanyabiashara wengi.
Mkutano huo
umefanyika Dar es Salaam ambapo ulihusisha Uongozi kutoka Benki ya
Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Wataalamu
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wataalamu kutoka Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
No comments :
Post a Comment