
Aliyepo kulia ni
Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki,Liberat Mfumukeko akisaini
mkataba wa EURO milioni 10 na Balozi wa umoja wa nchi za Ulaya nchini
Tanzania.Manfredo Fanti (aliyepo kushoto)kwa ajili ya kuimarisha ulinzi
na usalama katika nchi hizo.
******************************
Jumuiya ya Afrika Mashariki
imesaini mkataba wa EURO milioni 10 na umoja wa nchi za Ulaya kwa
ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi uanachama wa jumuiya
hiyo.
Mkataba huo
umesainiwa mapema leo katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo na
Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki ,Liberat Mfumukeko na
Balozi wa umoja wa nchi za Ulaya Tanzania ,Manfredo Fanti.
Akizungumza wakati wa
kusaini mkataba huo ,Katibu mkuu wa EAC ,amesema kuwa, fedha hizo
zimetolewa na jumuiya ya umoja huo ili kuziwezesha nchi wanachama
kukabiliana na changamoto ya usalama ambayo imekuwa na kikwazo kikubwa
Cha maendeleo katika nchi hizo.
Ameshukuru jumuiya
hiyo kwa msaada huo ambao umekuja muda muafaka na kuongeza kuwa, jumuiya
hiyo itaendelea kushirikiana kwa ukaribu Sana katika nyanja mbalimbali
za maendeleo.
Hata hivyo ,Mfumukeko
amesema kuwa,jumuiya hiyo ya nchi za Ulaya wamekuwa washirikiana kwa
muda mrefu na jumuiya hiyo ambapo katika kipindi cha miaka mitano
wamekwisha kutoa kiasi Cha EURO milioni 85 .
Kwa upande wake
,Balozi wa jumuiya ya umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Manfredo Fanti
amesema kuwa, wataendelea kusaidia jumuiya hiyo katika maswala
mbalimbali ya maendeleo .
“tumekuwa tukisaidia
jumuiya ya Afrika Mashariki katika miradi mbalimbali tangu mwaka 2007
ambayo imeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo na kuondokana
na changamoto mbalimbali zinazowakabili.”amesema Balozi huyo.
No comments :
Post a Comment