
Afisa Mahusiano ya jamii wa
TPDC Eugene Isaya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
wakati wa maonyesho ya bidhaa kwa wawekezaji wa viwanda Mkoa wa Pwani
(PICHA VICTOR MASANGU)
…………………….
SHIRILA la maendeleo ya petroli
Tanzania (TPDC) katika kukabiliana na changamoto ya uagizaji wa mafuta
kutoka nje ya nchi imekuja na mpango kabambe wa miradi mikakati
mitatu kwa ajili ya kufanya utafiti wa uchimbaji wa visima vya mafuta
katika mikoa ya
Tabora,Simiyu, pamoja na singida lengo ikiwa ni
kuipunguzia serikali ya awamu ya tano kutumia gharama kubwa katika
suala zima la uagizaji.
Hayo yalibainsihwa na Afisa
Mahusiano ya jamii wa TPDC Eugene Isaya wakati wa maonyesho ya bidhaa
za wawekezaji wa viwanda katika Mkoa wa Pwani, ambapo pia amebainisha
kuwa lengo lao linguine ni kuweza kutanua wigo katika kuzalisha gesi
asilia katika maeneo mbali mbali nchini ambayo itakuwa ni mkombozi
mkubwa kwa wananchi kuondokana na mtumizi ya ukataji wa miti ovyo.
Kwa upande wake Afisa uhusino wa
kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Latipher Kigoda amesema kwamba lengo
kubwa ni kuwasimamia na kuwaunganisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi
ikiwemo kutanagaza fursa mbali mbali zilizopo kwenye kilimo pamoja na
kuongeza thamani katika mazao ya biashara sambamba na kuwa na vifaa tiba
ambavyo vinazalisha ndani ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye amepokea jopo la wawekezaji saba
Kutoka jimbo la hebeyi kutoka nchini na kuwakabidhi mwongozo wa
uwekezaji wa Mkoa ambao utaweza kuonyesha fursa mbali mabli ambazo
zinapatikana katika halmashauri zote tisa lengo ikiwa ni kuwapatia
maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa kuzalisha chuma,nondo na saruji.
No comments :
Post a Comment