Waziri wa Viwanda na Biashara
Innocent Bashungwa (aliyeshika uzi) akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa
Kiwanda cha Nyuzi Tabora Pascal Jotham (mwenye shati nyeusi) leo
alipokuwa Mkoani Tabora kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo
hauridhishwa na utendaji wa kiwanda hicho na kuahidi kupitia Mkataba wa
Ubinafishaji wake.
Waziri wa Viwanda na Biashara
Innocent Bashungwa (katikati ) akiwa ameshika mmoja ya kitambaa
kilichozalishwa na Kiwanda cha Nyuzi Tabora wakati wa ziara yake Mkoani
Tabora jana ya kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na
utendaji wa kiwanda hicho na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji
wake.
Waziri wa Viwanda na Biashara
Innocent Bashungwa(kushoto) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora
Komanya Kitwala(kulia) wakati wa ziara yake Mkoani Tabora jana ya
kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa
kiwanda cha Nyuzi Tabora na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji
wake.
***********************
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI itapitia mkataba wa
ubinafsishaji wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora (New Tabora Textile
Tanzania Limited) baada ya kutoridhishwa utendaji wa uzalishaji ili
kuchukua hatua
mapema ambazo zitasaidia kufanyakazi kwa kiwango chake
endapo itabainikiwa wawekwenda kinyume kwa masharti yaliyomo.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Waziri wa Viwanda na Bisahara Innocent Bashungwa wakati wa ukaguzi wa
viwanda mbalimbali mkoani Tabora na kukuta kiwanda cha Nyuzi Tabora
kikiwa katika uzalishaji mdogo wakati pamba ya wananchi imejaa mitaani.
Alisema kiwanda hicho kingekuwa
kinafanyakazi kulingana na uwezo wake kingesaidia sana kupunguza tatizo
la ununuzi wa pamba ya wakulima kususua na kingeongeza uzalishaji wa zao
hilo na kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa.
Bashungwa alisema kwa kuwa Mmiliki
wa Kiwanda hicho ameonekana kuwa na uwezo mdogo na hivyo awe tayari na
maamuzi ambayo yatafikiwa baada ya kuangalia mkataba na vigezo
alivyopewa wakati ubinafishaji na ikibainika amekiuka Serikali itachukua
hatua ili kuongeza tija na utendaji kazi wake.
Alisema wakati wa Mwekezaji huyo
na wengine kuendelea kukalia viwanda ambavyo vilitarajiwa kuzalisha kwa
ajili ya kukuza uchumi na kutengeza ajira umekwisha na Serikali
itachukua hatua.
“Tutangalia Sheria inasemaje na
mkataba mlioingia …ili kuangalia njia bora ya kukifanya kiwanda hiki
kifanye kazi kwa ajili ya mustakabali mzuri wa wakazi wa Tabora na nchi
kwa ujumla” alisema.
Aidha Waziri huyo alivitaja
Viwanda vingine ambavyo uzalishaji na utendaji wake sio mzuri ni pamoja
na Mwatex na Mutex ambavyo navyo mikataba ya ubinifsishaji wake
itachunguzwa kwa ajili ya kuchukua hatua kuvinusuru.
Awali Mbunge wa Tabora Mjini
Emmenuel Mwakasaka alisema toka mwaka jana alipotembelea Kiwanda hicho
hakuna maendeleo yoyote ambayo yamefanyika na kukifanya kutokuwa na tija
kwa vijana na wakazi wa Tabora.
Alisema toka mwaka jana hakuna ajira hata moja iliyoongezeka zaidi ya mfanyakazi mmoja.
No comments :
Post a Comment