Ramani ya Nyumba za Mji mpya kwahani utakaogharimu kiasi cha Shil,Bilioni miambili hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
Baadhi ya Wageni waalikwa
waliohudhuria katika hafla ya utiaji saini Ujenzi wa Mji mpya wa
Kwahani hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango Iddi Haji Makame (kushoto)akitiliana saini na Meneja Mkuu wa
Kampuni ya ESTIM Construction co.ltd Girdhar M,Pindolia kuhusiana na
Ujenzi wa Mji mpya wa Kwahani hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango Iddi Haji Makame (kushoto)wakikabidhiana hati ya saini na
Meneja Mkuu wa Kampuni ya ESTIM Construction co.ltd Girdhar M,Pindolia
kuhusiana na Ujenzi wa Mji mpya wa Kwahani hafla iliofanyika muembe
njugu Zanzibar.
****************************
Na Rahma Khamis Maelezo 2/10/2019
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Iddi Haji Makame amewataka
wananchi
wa Kwahani kutokua na wasiwasi kwa kuvunjiwa nyumba zao kwani Serekali
ina dhamira ya dhati ya kuwajengea nyumba bora na za kisasa
Ameyasema katika
eneo litakalojengwa mji mpya wa nyumba za kisasa Kwahani wakati wa hafla
ya kutiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa nyumba hizo Estim
Construction LTD ya Dar es salaam .
Amesema kuanza
kwa ujenzi wa awamu ya kwanza ya nyumba tano za ghorofa nne kila moja
na maduka eneo eneo la chini ni uamuzi wa Serekali wa kuwaondoshea
wananchi mazingira ya zamani na kuwawekea ya kisasa.
Aliwaeleza
wananchi wa Kwahani kwamba Kampuni iliyopewa kazi za ujenzi wa mji mpya
Kwahani inauwezo mkubwa na wamekubaliana watakamilisha kazi hiyokwa
kipindi cha mwaka mmoja.
Amewashauri
kuendelea kuvuta subira katika kipindi hicho cha mpito huku wakiweka
matumaini ya kuishi katika mazingira bora na yakisasa.
MsimamizI wa
ujenzi wa nyumba hizo Lazaro Peter amewataka wnanchi wa eneo la Kwahani
kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi ili kazi ziweze kwenda kwa kasi na
zikamilike kwa muda uliopangwa.
Aliwapa matumaini
makubwa wananchi waliovunjiwa nyumba zao kwamba watapata nyumba bora na
za kisasa katika kipindi cha muda mfupi ujao.
Sheha wa Shehia
ya Kwahani Machano Mwadini Omar ameishauri Kampuni ya ujenzi wa nyumba
hizo kuwatumia vijana wa eneo hilo katika kazi zisizohitaji utaalamu ili
nao waweze kufaidika na mradi huo.
Alieleza kuwa
nyumba zilizovunjwa kwa ajili ya kupisha ujenzi mpya zilikuwa na vijana
wengi waliokuwa wakiendesha shughuli zao za maisha na hivi sasa hawana
kazi maalum hivyo iwapo watapatiwa kazi wakati wa ujenzi zitawasaidia
kimaisha
Baadhi ya
wananchi waliovunjiwa nyumba Ali Hamad Haji na Hija Sudi Juma wamesema
kuwa kuvunjiwa kwa nyumba zao imeleta shida kidogo lakini wataendelea
kuvuta subira na kuitaka Serekali ifanye uadilifu wakati ujenzi
utakapokamilika.
Aidha
wameipongeza Serekali kwa hatua waliochukua ya kupatiwa mtaji wa
kutafuta makazi ya muda huku wakisubiri makazi mapya ya kisasa
yatakayowatoa katika hali ya unyonge.
Katika utiaji
saini Serikali iliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Iddi
Haji Makame na Kampuni ya Estim Construction Co. LTD LTD iliwakilishwa
na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Girdhar Pindolia
No comments :
Post a Comment