*****************************
Na Silvia Mchuruza;
Kagera;
Vyandarua vyenye
viuatirifu vya kuuwa mbu waenezao maralia vipatavyo 348,380 vimeanza
kugawiwa katika shule zote za msingi zipatazo 981 katika Mkoa wa Kagera.
Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Kagera, Marco Mbata, akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa huo amesema
kuwa, zoezi la kugawa chandarua limeanza septemba 30 Mwaka huu na
litaisha Octoba 10 mwaka huu.
Mganga Mbata
ameongeza kwamba, wanafunzi wametumika kama njia ya kufikisha chandarua
kwenye familia na kuwa wanafamilia wanapaswa kuvitumia kwa malengo
yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Na kwamba ugawaji huo kitaifa ni awamu ya saba na katika mkoa wa Kagera ni awamu ya tatu.
Kwa upande wa mkuu wa
mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameeleza kuwa,
jitihada za serikali ni kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa na kuwa
mwaka 2015/2016 maambukizi yalikuwa ni 41% na mwaka 2017/2018 maambukizi
ya maralia yalikuwa 15.4%.
Aidha Brigedia Gaguti
amesema dhamira ya serikali ni kufikia mwaka 2020 maambikizi ya Maralia
yawe chini ya asilimia 1 na malengo ya kitaifa kufikia mwaka 2030
ugonjwa wa maralia uwe umetokomezwa kabisa.
Hata hivyo mradi huo
unatekelezwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali kwa ufadhiri wa serikali ya Marekani kupitia shirika la
misaada la watu wa marekani USAID.
Kauli mbiu ” Zero Maralia inaanza na mimi”
No comments :
Post a Comment