Marufuku Kufanya kazi ya kuchuna,kuwamba na kuhifadhi ngozi,bila kuwa na leseni au
kusajili eneo la biashara ya ngozi.
Haya yamebainishwa leo jijini
Arusha na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo na Usalama wa
chakula Bw.Gabriel Bura wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa
wachunaji.
”Hivyo ni marufuku kuchuna,kuwamba
au kuendesha biashara ya ngozi katika eneo husika bila kuwa na leseni
au kusajiliwa vinginevyo hatua kali zitachukuliwa kwa yule atakayefanya
kazi ya ngozi bila kuwa na leseni au kusajiliwa kisheria”amesema Bw.Bura
Kaimu Mkurugenzi huyo ameitaja
sheria inayomtia matatani atakaye fanya kazi ya ngozi bila kuwa na
leseni au kusajiliwa eneo lake la kazi atashitakiwa chini ya Sheria ya
ngozi namba 18 ya mwaka 2008.
Aidha kaimu mkurugenzi
huyo,amesema wanaopata leseni na kusajiliwa ni lazima wapatiwe mafunzo
kwanza kabla ya kuomba leseni na usajili wa taaluma ya teknolejia ya
utayarishaji bora wa zao la ngozi.
Mkurugenzi huyo,ameendelea kuleza
kuwa ni matarajio yake kuwa baada ya mafunzo haya anategemea makubwa
kuhusu mabadiliko ya ubora wa zao la ngozi utakuwa na tija kulingana na
ulewa wa wadau katika mafunzo waliyoyapata na hatimaye kuchangia
kikamilifu katika pato la Taifa.
No comments :
Post a Comment