Mkurugenzi wa TRC Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutiliana
saini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa mafunzo, utafiti na
kuendeleza matumizi ya teknolojia, Dar es Salaam Septemba 11, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (kulia) na Mkuu wa Taasisi ya
Teknolojia Dar es Salaam Prof. Preksedis Ndomba (kushoto) wakitia saini
Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa mafunzo, utafiti na kuendeleza
matumizi ya teknolojia, Dar es Salaam Septemba 11, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (kulia) na Mkuu wa Taasisi ya
Teknolojia Prof. Preksedis Ndomba (kushoto) wakibadilishana Makabrasha
ya Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kutiliana saini katika ukumbi wa
mikutano ofisi ya Makao makuu TRC Dar es Salaam Septemba 11, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (kulia) na Mkuu wa Taasisi ya
Teknolojia Dar es Salaam Prof. Preksedis Ndomba (kushoto) wakionesha
Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kutiliana saini ushirikiano wa
mafunzo, utafiti na kuendeleza matumizi ya teknolojia, Dar es Salaam
Septemba 11, 2019.
…………………
Shirika la Reli Tanzania – TRC
limetiliana saini mkataba na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam – DIT
kwa lengo la kushirikiana katika kutoa mafunzo, kufanya utafiti, na
kuendeleza
matumizi ya teknolojia katika huduma za usafiri wa reli,
makubaliano yamefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makao Makuu TRC jijini
Dar es Salaam Septemba 11, 2019.
Makubaliano hayo yametiliwa saini
kati ya Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa na Mkuu wa
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Prof. Preksedis Ndomba pamoja na
wanasheria kutoka pande zote mbili ambapo hafla hiyo fupi imehudhuriwa
na Wakuu wa Idara mbalimbali kutoka TRC, wawakilishi kutoka DIT na
waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania ameeleza dhumuni la makubaliano hayo ni kuwa ni kutokana na
mabadiliko yanayotarajiwaa kutokea katika Shirika hususani katika
huduma, amesema kuwa matumizi ya teknolojia ni muhimu kwa kuwa tayari
Shirika linasimamia miradi mikubwa ukiwemo wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa –
SGR, Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP na ukarabati wa Mabehewa hivyo
kuwa na wataalamu wa kutosha watakaoleta chachu katika matumizi ya
teknolojia ni muhimu.
“TRC tuko kwenye mageuzi na mageuzi yanakuja na teknolojia na vitu vipya, tunajenga reli ya kisasa – SGR kwahiyo tunahitaji kujua mifumo ya uendeshaji jinsi ilivyo kwahiyo sisi tumelikaribisha hili,” alisema Kadogosa
“TRC tuko kwenye mageuzi na mageuzi yanakuja na teknolojia na vitu vipya, tunajenga reli ya kisasa – SGR kwahiyo tunahitaji kujua mifumo ya uendeshaji jinsi ilivyo kwahiyo sisi tumelikaribisha hili,” alisema Kadogosa
Naye Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia
Dar es Salaam amesema kuwa hatua hiyo imekuja ikiwa ni sehemu ya
maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alizitaka
taasisi, Mashirika na serikali kufanya mageuzi ya teknolojia hivyo
Taasisi hiyo ikaamua kuzishirikisha taasisi, serikali na makampuni
katika kutoa mafunzo kwa wanafunzi wake, pia amesema kuwa TRC ni taasisi
ya kimkatati kwa ajili ya kujifunza
“tunaiona TRC kwa ukubwa wake, umaarufu wake na historia yake ni darasa moja kubwa sana si kwa wanafunzi tu hata kwa wafanyakazi, TRC ni taasisi ya kimkakati ambavyo tunaweza kujifunza” alisema Prof. Ndomba
“tunaiona TRC kwa ukubwa wake, umaarufu wake na historia yake ni darasa moja kubwa sana si kwa wanafunzi tu hata kwa wafanyakazi, TRC ni taasisi ya kimkakati ambavyo tunaweza kujifunza” alisema Prof. Ndomba
No comments :
Post a Comment