Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe akisalimiana na wahitimu wa Akademi ya
Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) katika
viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni
miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo
maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika.
Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi
pampja na mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana
Naibu waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na wahitimu wa
Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy)
katika viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka
Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki
mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice
Afrika. Kutoka kulia ni Wilson Nkya, Grace Mgaya, Jane Moshi, Sarah
Kimario na Jamal Mohamed.
Naibu Spika Dr. Tulia Ackson
(katikati) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice
(MultiChoice Talent Factory Academy) nje ya ukumbi wa bunge jijini
Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi
60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa
filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kushoto ni Jane
Moshi, Sarah Kimario, Jamal Mohamed na Wilson Nkya
Mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice
Tanzania Johnson Mshana (wa pili kushoto) akiwatambulisha wahitimu wa
mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu kwa Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe (Kushoto) mara baada ya wahitimu
hao kuhudhuria kikao cha bunge kama wageni maalum wa waziri. Wanafunzi
hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika
walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na
MultiChoice Afrika kupitia program yake ya MultiChoice Talent Factory.
Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi
pampja na Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Grace Mgaya
…………………..
- Tulia, Mwakyembe, Shonza, Mavunde wawapa neno
- Katibu Mkuu asisitiza ahadi ya serikali kushirikiana na wadau
Wanafunzi wanne waliohitimu hivi
karibuni mafunzo maalum ya uzalishaji filamu chini ya
programu ya
MultiChoice Talent Factory wamehudhuria kikao cha bunge la Tanzania kama
wageni maalum wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Katika ziara hiyo pia
wanafunzi hao walikutana na wadau mbalimbali akiwemo naibu spika Dr.
Tulia Akson waziri Dr. Harrison Mwakyembe, naibu waziri Juliana Shonza,
naibu waziri Anthony Mavunde na katibu mkuu wa wizara Suzan Mlawi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
na wahitimu hao katika viwanja vya bunge jijini Dodoma, viongozi hao
waliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo maalum waliyoyapata katika
kuleta mapinduzi ya tasnia ya filamu hapa Tanzania.
Naibu waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na
wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory
Academy) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4
kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika
walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na
MultiChoice Afrika. Kutoka kulia ni Wilson Nkya, Grace Mgaya, Jane
Moshi, Sarah Kimario na Jamal Mohamed.
Kwa pamoja wamekiri kuwa
tasnia ya filamu ni moja ya tasnia zinazokuwa kwa haraka hapa nchini
hivyo ni muhimu wanatasnia wawe na mafunzo ya kutosha na yanayoendana na
wakati ili iweze kupambana na nchi nyingine katika soko la filamu
ulimwenguni huku tukihakikisha kuwa kazi zetu zinaakisi mila, desturi,
utamaduni na uzalendo wetu.
Naibu Spika Dr. Tulia
Ackson (katikati) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya
MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) nje ya ukumbi wa bunge
jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa
wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya
uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka
kushoto ni Jane Moshi, Sarah Kimario, Jamal Mohamed na Wilson Nkya
Akizungumza na wanafunzi hao
baada ya kumtembelea ofisini kwake, Katibu Mkuu Suzan Mlawi amesisitiza
ahadi ya serikali kushirikiana na wadau wa tasnia mbalimbali ili
kuharakisha ukuaji wa tasnia hizo. Amesema ushirikiano kati ya serikali
na wadau ni muhimu na kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kuwa sera
na kanuni zinaboreshwa ili kuakisi hali halisi ya ukuaji wa tasnia ya
filamu.
Wanafunzi hao wanne – Wilson Nkya,
Jane Moshi, Jamal Mohamed na Sarah Kimario wamehitimu mafunzo maalum ya
mwaka mmoja yanayofadhiliwa na MultiChoice ambapo vijana 60 kutoka kote
barani Afrika huchaguliwa kwa mafunzo hayo kutoka nchi mbalimbali.
Programu hiyo ina vituo vitatu vya mafunzo ambapo kwa upande wa kusini
mwa Afrika kipo Lusaka Zambia, kwa Afrika Mashariki na kati kipo Nairobi
Kenya na kwa Afrika Magharibi Lagos Nigeria.
Mkuu wa Mahusiano wa
MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wa pili kushoto) akiwatambulisha
wahitimu wa mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu kwa Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe (Kushoto) mara baada
ya wahitimu hao kuhudhuria kikao cha bunge kama wageni maalum wa waziri.
Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka
bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu
yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika kupitia program yake ya
MultiChoice Talent Factory. Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal
Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi pampja na Afisa Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania Grace Mgaya
Awamu ya pili ya program hii
itaanza mwezi Octoba 2019 ambapo wanafunzi wengine 60 watapata mafunzo
hayo. Tanzania kwa mara nyingine tena itapeleka wanafunzi wanne.
No comments :
Post a Comment