
***************
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT),Prof.Florens Luoga amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Dunia kanda ya ya Afrika (Africa Group 1), Bi.Anne Kabagambe ofisini
kwake jijini Dar es Salaam.
Gavana Luoga amemwelekeza Bi.Kabagambe hatua mbalimbali ambazo
BoT inachukua kuhakikisha kuna ukuaji wa uchumi,kuimarisha sekta ya
mabenki,mifumo ya malipo na huduma jumuishi za kifedha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Kuu ya Dunia
aliipongeza BoT kwa hatua mbalimbali inazochukua kutekeleza sera ya
fedha na na kueleza utayari wa Benki ya Dunia kushirikiana katika nyanja
mbalimbali za kimaendeleo.
Manaibu Gavana wa BoT, Dkt.Yamungu Kayandabila na Dkt.Benard
Kibesse na Mshauri Mwandamizi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji huyo,
Bw.Zarau Kibwe, walihudhuria mazungumzo hayo.
No comments :
Post a Comment