
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Munge, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
akiwa amepanda juu kukagua maendeleo ya ujenzi wa tenki la maji la Mradi
wa Maji wa Tella Mande, wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Maji wa Tella Mande, wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
akizungumza na Mkandarasi wa Kampuni ya Mbeso Construction Ltd
(katikati) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa
Munge, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Siha, Onesmo Buswelu.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
akizungumza na watumishi wa Makao Makuu ya Ofisi za Bonde la Mto Pangani
(hawapo pichani), mkoani Kilimanjaro. Katikati ni Afisa Maji wa Bonde
la Pangani, Segule Segule na kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Kunusuru
Vyanzo vya Maji Kupitia Matumizi Bora ya Ardhi (SLM), Mhandisi
Maxmillian Sereka.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
akiwa kwenye kikao na watumishi wa Makao Makuu ya Ofisi za Bonde la Mto
Pangani, mkoani Kilimanjaro.
……………….
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
amesema Serikali imedhamiria kutumia zaidi wataalam wake wa ndani katika
utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji baada ya mafanikio makubwa
yaliyopatikana kwa kazi walizopewa.
Amesema maamuzi hayo yamekuja
baada ya wataalam hao kufanya kazi nzuri, zinazochukua
muda mfupi
kukamilika, zenye viwango na kwa gharama nafuu ukilinganisha na
wakandarasi ambao kazi zao zimekuwa na changamoto mbalimbali
zinazokwamisha juhudi za Serikali kumaliza tatizo la maji.
Naibu Waziri Aweso amesema kwa
muda mrefu Serikali imekuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wa
miradi ya maji nchini kutokana na ubabaishaji wa wakandarasi licha ya
kutumia fedha nyingi kwa dhumuni la kufikisha huduma ya maji kwa kila
mwananchi.
‘‘Tumekuwa na utaratibu wa kuwapa
kazi Wataalam Washauri ya usimamizi wa ujenzi wa miradi kwa gharama
kubwa, lakini wamekuwa wakishirikiana na wakandarasi kuihujumu Serikali
kwa kutotimiza wajibu wao na kuingizia Serikali hasara kubwa’’, Naibu
Waziri Aweso amefafanua.
‘‘Baada ya kugundua tatizo hilo
tukaamua kutumia wataalam wa ndani waliopo kwenye mamlaka za maji,
wahandisi wa mikoa na wilaya kwenye miradi mingi iliyokuwa imekwama au
ujenzi wa miradi mipya kwa gharama ndogo na kupata mafanikio makubwa,
Aweso ameeleza.
Akieleza kuwa baadhi miradi mingi
iliyosimamiwa au kutekelezwa na wataalam wa ndani katika mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya na Kanda ya Ziwa imekuwa na mafanikio
makubwa, jambo ambalo limeifanya Serikali kudhamiria kutumia zaidi
wataalam hao na kuachana na wakandarasi wababaishaji kwa lengo la kupata
matokeo mazuri.
Awali, Naibu Waziri Aweso
alichukua hatua ya kumkamata Mkandarasi wa Kampuni ya Mbeso Construction
Ltd kwa sababu ya kusuasua kwa ujenzi wa miradi ya maji ya Munge na
Tella Mande iiliyopo katika Wilaya za Siha na Moshi, mkoani Kilimanjaro
bila sababu za msingi.
Hatua hiyo imekuja baada ya Aweso
kukagua Mradi wa Maji wa Munge, wilayani Siha na kutoridhiswa na kasi ya
mkandarasi na muda wa utekelezaji wake ukiwa umebaki mwezi mmoja na
kazi ikiwa ni asilimia 25 hali akiwa hana madai yoyote ya fedha kwa
Serikali.
No comments :
Post a Comment