
****************
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
MKUU wa mkoa wa
Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ,amesisitiza kwamba ,Tanzania hususan
mkoani Pwani ni salama kwa uwekezaji na amekemea propaganda na uvumi
unaoenezwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa kuwa hakuna
uwekezaji unaoendelezwa.
Aidha amewaasa
,wawekezaji na wenye viwanda kuhakikisha wanasajili namba za utambulisho
ya mlipa kodi (TIN no) kwa meneja wa mamlaka ya mapato (TRA )mkoani
hapo ili hali kuongeza pato la mkoa.
Ndikilo alitoa rai hiyo, wakati alipokwenda kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitano vilivyopo wilayani Mkuranga.
“Rais dkt.John Magufuli amekuwa akisisitiza
uwekezaji na ujenzi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati, sasa akitokea
mtu kukwamisha jitihada hizo anakuwa halitakii mema Taifa, :”‘Pia mkoa
wetu kupitia halmashauri umetenga maeneo hekta 22,937 kwa ajili ya
uwekezaji ,nawaomba wawekezaji waje kuwekeza .”alifafanua Ndikilo.
Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa aliwataka wenye
viwanda kujali mikataba,haki,maslahi ya wafanyakazi kwa kuzingatia
sheria pamoja na kuwapa likizo na kuwawekea vitendea kazi .
Awali mkurugenzi wa kiwanda kinachozalisha
matofali yenye ubora (Shaffa Ltd) kitongoji cha Kiguza, Suleiman Amour
alibainisha ,ujenzi wa kiwanda umeanza 2018 kinatarajia kitakamilika
mwaka 2019.
Amour alisema, lengo la mradi huo ni kuongeza
wigo katika sekta ya ujenzi ,na ujenzi utagharimu sh.bilioni 15.3 hadi
kukamilika ambapo itatoa ajira 200 mradi ukikamilika.
Kwa upande wake,
msimamizi usafirishaji wa kiwanda cha super meals (Cool Blue) kilichopo
Vianzi, Charles Malini alisema, ujenzi wa kiwanda umegharimu bilioni
2.7, kuna ajira 50 ,kinalisha maji ya kunywa ya chupa kwa matumizi ya
majumbani na ofisini ambapo wanazalisha ujazo mbalimbali kuanzia nusu
lita hadi lita 18.
Alitaja changamoto zinazowakabili ni kukosa umeme wa uhakika na miundombinu ya barabara isiyo rafiki .
Ndikilo alizungumzia
tatizo la barabara na kuwaeleza ,ataangalia namna ya kuingiza hoja hiyo
katika kikao cha barabara kijacho ili kiweze kutetea ipandishwe hadhi
ihudumiwe na Tanroads.
Meneja wa shirika la
umeme-TANESCO wilayani Mkuranga, Octavian Mmuni alisema tatizo la
kukosekana umeme wa uhakika hutokana na maboresho yanayofanyika mara kwa
mara.
Mmuni alieleza, kwa sasa shirika hilo limetenga sh.milioni 261 ili kusaidia kubadili nguzo na nyaya chakavu.
Viwanda vingine
vilivyowekwa mawe ya msingi katika wilaya hiyo ,ni kiwanda
kinachozalisha zana za uvuvi Taxtrade T2 Ltd ,cha nyaya za umeme -Plug
Ltd na kiwanda cha kutengeneza masufulia cha Maxima.
No comments :
Post a Comment