NA
K-VIS BLOG
WIMBO
wa “Tetema kama umepigwa shoti”
ulioimbwa kwa ushirikiano kati ya mwanamuziki nyota barani Afrika Diamond
Platnamz na Rayvanny (pichani juu) umezua gumzo nchini Kenya baada ya Mamlaka ya nchi hiyo
kuupiga marufuku kuimbwa maeneo ya wazi (hadharani).
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu Nchini Kenya, Dkt. Ezekiel Mutua amsema kuwa ni
jambo la kusikitisha kuwa hata viongozi wa kitaifa wamekuwa wakiimba na kucheza
wimbo huo wa Tetema licha ya kuwa na
maudhui yenye kuvunja maadili ya Wakenya.
“Inasikitisha hata viongozi wetu wa kitaifa wamekuwa wakiimba na
kucheza nyimbo za Tetema na Wamlambez hadharani, sasa nyimbo hizi zimepigwa
marufuku kuimbwa nje ya Klabu (clubs) na Baa, zinaujumbe (maudhui) machafu na
hazifai kwa matumizi ya umma hazifai
kutazamwa na watoto na kiukweli zinahamasisha ngono.” Alisema Dkt. Mutua
kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii za Tweetter na Facebook Agosti 27,
2019.
Hata hivyo katazo hilo la Dkt. Mutua, limezua mtiririko
wa maoni kutoka kwa Wakenya wengi wakisema katazo lake limechelewa na ndio
limechagiza wimbo huo kuwa maarufu miongoni mwa
Wakenya.
![]() |
| Dkt. Ezekiel Mutua |
Kwenye ukurasa wa Facebook wa Dkt. Mutua leo asubuhi
Agosti 28, 2019, jumla ya maoni 580 yametolewa huku mengi ya maoni hayo yakimweleza
kuwa amechelewa kutoa tangazo hilo na kwamba hivi sasa wimbo huo umekuwa maarufu
kama kama wimbo wa taifa wa Kenya.
Katika akaunti yake ya Tweetter, wasomaji 890 wamejibu
ujumbe wake (tweet) na kumnekuwa na maoni mchanganyiko mengi yakimkejeli kwa
katazo lake hilo.

No comments :
Post a Comment