KATIKA
hali isiyo ya kawaida mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameandamana
kuelekea katika Ubalozi wa Afrika ya Kusini nchini kushinikiza kuachiwa kwa
ndege ya ATCL inayoshikiliwa Jijini Johanesberg Afrika ya Kusini kwa amri ya
Mahakama.
Maandamano
hayo ambayo hayakufahamika yametokea
upande gani wa Jiji yaliwashirikisha watu mbalimbali wakiwemo waliojitambulisha
kama wanafunzi wa vyuo vya elimu ya Juu pamoja na wananchi wa kawaida waliodai wamechoshwa na vitendo vya kuihujumu
serikali ya awamu ya Tano.
Mabango
mbalimbali waliyobeba waaandamanaji hao yalionyesha kusikitishwa na kitendo cha
kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Afrika ya Kusini , nchi ambayo uhuru
wake umepatikana kwa msaaada wa Tanzania kwa kuwasaidia makazi na hata vifaa
waliokua wapigania uhuru wa nchi hiyo.
Mmoja
wa waandamanaji hao ambaye hakutaka kutaja majina yake , akiongea kwa uchungu
alisema Afrika ya Kusini imekua nchi isiyo na shukrani kabisa kwa kitendo cha
kuikamata ndege ya ATCL ambalo ndilo kwanza linatoka katika hali ya kuwa
taabani.
“Tumekuja
hapa kuwaambia wenzetu wa Afrika ya Kusini kwamba uungwana sio tu kulipa
fadhila kwa aliyekusaidia, bali hata matendo tu yanatosha, haiwezekani sisi
tumewasaidia wapate uhuru leo hii hawana hata aibu wanakamata ndege yetu tena
kwa sababu zisizokua na msingi” Alisema mmoja wa waandamanaji hao.
Mingoni
mwa mabango waliyobeba yalisomeka ‘Turudishieni ndege yetu na sisi tuwarudishie
makaburu uhuru wao maana mmeshindwa kuwa wasataarabu’ lingine lilisomeka ‘ Waafrika
ndio maana tunadharaulika duniani kwa kufanya mambo ya hovyo.
Kwa
upande wake Sadik Ramadhan aliyekua anazungumza kwa jazba alisema waafrika ya
kusini ni rafiki zetu kitendo cha kushirikiana na mzungu mmoja kuihujumu
Tanzania ni kitendo ambacho hakikubaliki
kabisa, alisema Rais Ramaphosa alipokuwa nchini kwenye mkutano wa SADC
aliwahakikishia watanzania kwamba undugu wa nchi hizi utaendelea na hakuna hata
mtu mmoja wa kuuvunja.
Aidha
alisema lengo la maandamano hayo ya amani ni kumtaka Balozi atoke na aeleze ni
hatua gani zinazoendelea za kuhakikisha ndege ya watanzania inarudi kwani
imenunuliwa kwa kodi za wananchi tena wananchi masikini wanaopambana kuinua nchi
yao.
Huku
wakiimba wimbo kwamba wamemsaliti mzee Mandela waandamanaji hao walisema inatia
uchungu sana kuona taifa lililosaidiwa na Tanzania ndio sasa linakua mstari wa
mbele kuhujumu mali zake jambo ambalo wamesema halikubaliki.
Maandamano
hayo ambayo yalizua taharuki kwa takriban nusu saa, yalizimwa na Jeshi la
polisi kwa kuwataka waandamanaji hao kuondoka kwa madai suala hilo linaendelea
kushughulikiwa kwa mujibu wa sharia na taratibu za kidiplomasia.
Baada
ya kuamriwa kuondoka waandamanaji walitawanyika wakiendelea kuimba kwamba ujume
umefika na kilichobaki wanasubiria ndege yao na kama haitaachiwa watafanya
ubalozi huo ushindwe kutekeleza kazi zake za kila siku kwani wataandamana mpaka
kieleweke.
Kwa
upande wake kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa
alipofika kwenye ubalozi huo aliwataka waandamanaji kufuata sharia na
kutojichukulia sharia mkononi kwani wanaweza kushitakiwa, aidha Jeshi la Polisi
liliwatia nguvuni baadhi ya waandamanaji hao.
Hadi
maandamano hayo yanavunjwa hakuna kiongozi yeyote wa ubalozi huo aliyejitokeza
kusikiliza hoja za waandamanaji bali walijifungia ndani huku baadhi ya
wafanyakazi wakionekana kuchungulia madirishani kuona nini kinaendelea , na
wengine wakipiga picha kwa kutumia simu zao za kiganjani.
No comments :
Post a Comment