RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar
,wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara
hiyo juazia mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa
Ikulu Zanzibar , kushoto kwa Rais Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na kulia kwa Rais Katibu Mkuu Kiongozi na
Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.(Picha na Ikulu)
WAZIRI
wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali
akiwasirisha mutasari wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara
yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, kulia Katibu Mkuu Kiongozi
na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na
kushoto Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Hassan Khamis
Hafidh, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,
hayupo pichani.
MKURUGENZI
wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Ndg .Khatib Mwadin akijibu
swali wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti ya Mpango Kazi kwa
mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,
ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani kulia Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC) Dk. Said Seif Mzee
NAIBU
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Bi. Khadija Khamis
Rajab wa kwanza kushoto akisoma taarifa ya Utekelezaji Bajeti na Mpango
Kazi ya Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2018, wakati wa
mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na
Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
BAADHI
ya Watendaji wa Idara za Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar
wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa Wizara
yao kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, mkutano huo umefanyika
katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC)
Ndg Maalim Kassim Suleiman, akizungumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji
wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa mwezi wa
Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,
ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani.
MSHAURI
wa Rais Pemba Mhe.Dk. Maua Abeid Daftari akizingumza wakati wa mkutano
wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na
Viwanda Zanzibar uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, ukiongozwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali
Mohamed Shein. Hayupo pichani.
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akizungumza wakati
wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya
Biashara na Viwanda Zanzibar kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019,
uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Uongozi
huo pia, ulizitaja bidhaa zilizizothibitishwa ubora na kupatiwa alama
ya ubora ya (ZBS) kwa mwaka 2018/2019 ni maji ya kunywa ya (Zan Aqua),
mchele (Tulip) unaozalishwa nchini Pakistan, mchele wa (Ikram), unga wa
sembe (Mwangaza), Mikate ya slesi, maji ya kunywa (Pure life) na (Uhai),
mafuta ya nazi na mifuko.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
ameeleza kuwa nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuhakikisha
sauti za Wajasiriamali zinasikika na zinafanyiwa kazi ili kufikia
malengo waliyoyakusudia.
Rais
Dk. Shein aliyasema, Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa
Wizara ya Biashara na Viwanda wakati ilipowasilisha Mpango Kazi wa Julai
2018 hadi Juni 2019 sambamba na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa mwaka
2019/2020.
Alieleza
kuwa matajiri walio wengi duniani walianza na ujasiriamali hivyo ni
vyema wajasiriamali wakapewa kipaumbele katika shughuli zao
wanazozifanya ili waweze kupata mafanikio na kufikia malengo yao
waliyoyakusudia ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha kikamilifu katika
maonesho ya kibiashara ya ndani na nje ya nchi.
Alieleza
kuwa mbali ya matajiri hao duniani, hata hapa Zanzibar matajiri walio
wengi wameanza na ujasiriamali hivyo, si jambo la busara kuwabeza na
badala yake ni vyema wakapema kipaumbele na mashirikiano ya kutosha.
Aidha,
Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kuwasaidia wajasiriamali ili na wao
waweze kuwa wafanyabiashara wakubwa na kufikia malengo waliojiwekea
jambo ambalo limeiibua Serikali katika kuhakikisha inawatekelezea
matakwa yao na kuwashirikisha kikamilifu
Pamoja
na hayo Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi wa
Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kuwasilisha vyema Mpango Kazi wao na
kueleza kuwa utendaji wao pamoja na wafanyakazi wa Wizara hiyo ndio
uliopelekea kupata mafanikio
Hivyo,
Rais Dk. Shein aliutaka uongozi huo kuongeza kasi na kufanya kazi kwa
bidii ili mafanikio zaidi yaendelee kupatikana katika kuimarisha sekta
hiyo ambayo ina umhimu katika kuimarisha uchumi na kukzua sekta za
kijamii.
Rais
Dk. Shein alipongeza mafanikio makubwa yaliopatikana katika Wizara hiyo
chini ya uongozi wa Waziri wake Balozi Amina Salum Ali ambaye amefanya
juhudi kubwa ya kuiimarisha Wizara hiyo katika uongozi wake kwa
mashirikiano ya pamoja na watendaji wake.
Dk.
Shein aliutaka uongozi wa Wizara hiyo kuendelea kumsaidia Waziri wao
huyo kila mmoja kwa wakati wake na nafasi yake kwa lengo la kuimarisha
sekta ya biashara na viwanda kwani azma ya Serikali ni kuhakikisha
Zanzibar inakuwa kwenye ramani ya viwanda.
Alieleza
matumaini ya kuimarika kwa zao la mwani ambapo tayari kuna aina nne za
mwani hapa Zanzibar na kueleza kuwa hatua hiyo itapelekea kupata
mafanikio mazuri ya zao hilo ikiwa ni pamoja na mchakato wa kujenga
kiwanda cha mwani huko Chamanangwe Pemba.
Alieleza
kuwa Zanzibar ina historia kubwa ya kulima mazao mbali mbali yakiwemo
ya viungo vya chakula kwa muda mrefu, hivyo ni vyema mazao hayo
yakaimarishwa ikiwa ni pamoja na kuwashajiisha wakulima kuyalima
vikiwemo viungo kama pilipili hoho.
Rais
Dk. Shein alisisitiza haja ya kulima kwa wingi kwa viungo vya chakula
kwa sababu vimekuwa vikipendwa sana nje ya nchi hivyo ni vyema kilimo
hicho kikaimarishwa.
Aidha,
alieleza kufarajika kwake na uongozi wa Wizara hiyo kwa kutumiwa alama
ya ubora ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) katika bidhaa mbali mbali
zinazozalishwa ndani na nje ya nchi huku akieleza azma ya Zanzibar kuwa
nchi ya viwanda.
Makamo
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alitoa pongezi kwa
uongozi huo na kuzipongeza juhudi za Waziri Balozi Amani Salum Ali za
kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika sekta ya viwanda na biashara
ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Mamlaka inayosimamia Viwanda vidogo
vidogo na Vya Kati (SMIDA).
Nae
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid
Yahya Mzee aliipongeza kazi nzuri ya uwasilishaji iliyofanywa na Wizara
hiyo huku akisisitiza haja kwa uongozi huo kuendeleza mashirikiano na
uadilifu.
Mshauri
wa Rais wa Zanzibar Pemba Dk. Maua Abeid Daftari kwa upande wake alitoa
pongezi kwa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) kwa kuendeleza zao la
mchaichai kisiwani Pemba kwani wananchi wengi wamehamasika na kuomba
wasaidiwe kuwekewa vinu karibu na sehemu wanazoishi.
Mapema Waziri
wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salaum Ali akiwasilisha muhtasari
wa utekelezaji Mpango Kazi wa Wizara hiyo alisema katika kipindi cha
mwaka 2018/2019 jumla ya tani 218,911 za chakula muhimu ukiwemo mchele,
sukari na unga wa ngano zilikuwepo kwa ajili ya matumizi ya soko la
ndani na kuifanya Zanzibar kuendelea kuwa na chakula cha kutosha cha
aina hizo katika kipindi chote.
Alieleza
kuwa sensa ya viwanda iliyofanyika mwaka 2016 ilionesha idadi ya
viwanda imeongezeka ambapo sukari imeongezeka kutoka tani 677
iliyozalishwa mwaka 2017 hadi tani 3,339 kwa mwaka 2018 sawa na ongezeko
la asimilia 79.7 na uzalishaji wa unga wa ngano nao uliongezeka kutoka
tani 25,196 mwaka 2017 hadi tani 26,963 mwaka 2018.
Balozi
Amina alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2018/2019, Shirika la
Biashara la Taifa limenunua karafuu tani 211.34 kwa jumla ya TZS Bilioni
2.9 ambapo pia uzalishaji wa mafuta ya mimea ulifikia kilo 40,955.3 kwa
jumla ya TZS bilioni 1.5.
Alieleza
kuwa Serikali inaendelea kununua karafuu kulingana na Sera ya Serikali
ya kununua kwa bei ya asilimia 80 ya bei ya kuuzia nje hata hivyo, msimu
mdogo wa karafuu kwa mwaka 2018/2019 ulipelekea kupungua kwa tani za
ununuzi wa karafuu.
Kwa
bajeti ya mwaka 2019/2020, alisema Wizara inakusudia kuimarisha maabara
za ZBS zilizopo Amani pamoja na kuimarisha miundombinu, vifaa vya
ukaguzi wa magari, kuliendeleza eneo la Nyamanzi sambamba na kuongeza
vifaa kwa ajili ya matamasha.
Alieleza
kuwa Wizara hiyo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Indonesia
inatarajia kufanya mafunzo ya ukulima wa mwani ulio na tija na kuanza
maandalizi ya kuanzisha kiwanda cha kusarifu mwani huko Chamanangwe
kisiwani Pemba.
Balozi
Amina, alieleza mpango wa Wizara wa kusimamia program maalum ya
wajasiriamali inayopata msaada kutoka mfuko maalum wa Nchi za Falme za
Kiarabu pamoja na mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisisitiza
kuwa ili kurahisisha ufanyaji biashara hapa Zanzibar, Wizara itaandaa
mfumo maalum wa Tehama ambao utatoa taarifa na huduma muhimu za usajili,
uwekezaji na leseni au vibali vinavyotakiwa kwa wawekezaji na
wafanyabiashara.
Pia,
uongozi huo ulieleza juhudi inazozichukua kwa wafugaji wa nyuki kwa
kuwapa mafunzo maalum wafugaji hao sambamba na kusimamia vyema ufugaji
huo kwa lengo la kupata asali yenye ubora na viwango vinavyohitajika
kitaifa na kimataifa.
Uongozi
huo pia, ulimpongezi Rais Dk. Shein kwa utaratibu mzuri alioweka wa
mikutano hiyo inayojadili Mpango Kazi wa Mawizara huku wakitumia fursa
hiyo kueleza sifa inazozipata Zanzibar kutoka kwa wageni wanaokuja
kuitembelea kutokana na amani, utulivu, upendo pamoja na maendeleo
yaliopo.
No comments :
Post a Comment