Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari leo Agosti 3, 2019, Mkuu wa mkoa wa
Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti akiwa kamati ya maandalizi
ya wiki ya Kagera katika kikao kilichofanyika katika ofisi za mkoa huo
zilizopo manispaa ya Bukoba,amewataka wananchi na wadau toka nje na ndani ya mkoa wa Kagera wakitakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika wiki hiyo.
Mkuu
huyo wa mkoa amewataka waandishi wa habari kupitia vyombo vyao vya
habari kuwaalika wadau mbalimbali wa uwekezaji pamoja na wananchi wote
wa nje na ndani ya mkoa wa Kagera kushiriki katika wiki ya uwekezaji
Kagera.
"Ndugu
wana habari wiki ya uwekezaji Kagera inatarajia kuanza Agosti 12, 2019,
ambayo itaanza na maonyesho ya bidhaa au fursa mbalimbali
zinazopatikana katika mkoa wa Kagera ambapo Tarehe 12-13/8/2019 na
maonyesho hayo yatafanyika katika uwanja wa Gymkhana uliopo katika
Manispaa ya Bukoba",amesema.
Gaguti
amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ndiye atafungua rasmi
kongamano la wadau wa uwekezaji litakalofanyika katika ukumbi wa Hotel
ya ELCT Bukoba.
Ameongeza
kuwa tarehe 15 Agosti 2019 kongamano la wadau wa uwekezaji litaendelea
ikiwa ni pamoja na maonyesho mbalimbali ambapo Agost 16 /2019 wiki ya
uwekezaji itafungwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Uwekezaji Mh. Angela Kairuki na mara baada ya kufunga rasmi wadau wa
uwekezaji watapata nafasi ya kwenda kutembelea vivutio vya Utalii pamoja
na fursa za uwekezaji zilizomo mkoani Kagera hadi Agosti 17 mwaka huu.
Aidha
Gaguti ameeleza kuwa wiki ya Kagera ni fulsa kwa wadau mbali mbali wa
uwekezaji kuja Kagera kuwekeza hasa katika sekta za kilimo kutokana na
misimu miwili ya mvua kwa mwaka lakini pia mazao mengi ya chakula na
biashara yanakubalika sana katika mkoa huu akitolea mfano zao la ndizi,
kahawa, vanilla, chai, kokoa na mazao ya chakula ni mahindi na maharage
huku fursa nyingine zikiwa ni uvuvi, ufugaji, viwanda, elimu, utalii na
utamaduni wa wananchi wa Bukoba.
Katika
hilo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika wiki hiyo ili
kuufungua mkoa wa Kagera kimtaji na kiuchumi na kutengeneza ajira za
vijana mkoani humo.
Pia
Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka taasisi zote za serikali na zisizokuwa za
serikali zilizopo mkoani hapa kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika
wiki ya uwekezaji ili kuonesha fursa walizonazo na kizitangaza kwa wadau
mbali mbali ambao wanatarajia kuhudhuria katika wiki hiyo kutoka ndani
na nje ya nchi.
Hata
hiyo mkoa huo unatarajia kuwapokea mabalozi wanne kutoka nchi jirani za
Congo, Kenya, Rwanda, Burundi, na Uganda sambamba na wafanyabiashara
kutoka mataifa jirani ili waungane na wafanya biashara wa hapa ili
kushirikiana kujenga uchumi endelevu, huku akitaja kauli mbiu ya wiki ya
uwekezaji Kagera kuwa ni "Kagera: Eneo la kimkakati kwa uchumi wetu na Afrika Mashariki".

No comments :
Post a Comment