KATIBU
Tawala wa wilaya ya Handeni Mwalimu Boniface Maiga akizungumza wakati
wa utambulisho wa mradi wa kuhamasisha uwajibikaji wa jamii na mamlaka
zinazohusika katika kuboresha elimu katika vijiji nane vya halmashauri
ya wilaya hiyo uliokwenda sambamba na mkutano wa wadau uliofanyika Kata
ya Mkata ambapo mradi huo unaendeshwa na asasi ya Tree of Hope chini ya
ufadhili wa Foundation for civil Society (FCS) kulia ni Diwani wa Kata
ya Mkata akifuatiwa na Mratibu wa Mradi wa Kuhamasisha uwajibikaji wa
Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu kwenye vijiji nane
Goodluck Malilo
Mratibu
wa Mradi wa Kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika
katika kuboresha elimu kwenye vijiji nane wilaya ya Handeni Goodluck
Malilo akizungumza
Mwezeshaji Wakili Richard Vicent akisisitiza jambo
Sehemu ya washiriki wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya washiriki wakifuatilia matukio mbalimbali
Mmoja wa washiriki akichangia
Mmoja wa washiriki akijitambulisha
Mratibu
wa Mradi wa Kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika
katika kuboresha elimu kwenye vijiji nane wilaya ya Handeni Goodluck
Malilo kushoto akiteta jambo na Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni
Mwalimu Boniface Maiga mara baada ya kufungua
WATUMISHI
wa Halmashauri wilayani Handeni mkoani Tanga wameonywa kuacha kufanya
vitendo vya ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa
kwenye maeneo yao kwani zitawatokea puani.
Hayo
yalisemwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mwalimu Boniface Maiga
wakati wa utambulisho wa mradi wa kuhamasisha uwajibikaji wa jamii na
mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu katika vijiji nane vya
halmashauri ya wilaya hiyo.
Utambulisho
huo ulikwenda sambamba na mkutano wa wadau uliofanyika Kata ya Mkata
ambapo mradi huo unaendeshwa na asasi ya Tree of hope chini ya ufadhili
wa Foundation for civil Society (FCS).
Alisema
kwamba sio ambao watabainika wamehusika kwenye kufanya ubadhirifu
wakifanya uchunguzi na wakibaini wamehusika watawashughulikia kwa mujibu
wa sheria na hakuna ambaye atasalimika
Katibu
Tawala huyo ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin
Gondwe alisema kwamba hawatakuwa tayari kuona fedha zinazopelekwa kwenye
maeneo yao na serikali huku zikihujumiwa hivyo watakuwa wakali kwa
kuhakikisha wahusika wanashughulikiwa.
“Niwaonye
watumishi ambao mnaofanya ubadhirifu kwenye miradi inayotelekezwa
kwenye maeneo yenu acheni tabia hiyo mara moja kwani hatutawavumilia na
hili niseme kwamba fedha ya serikali hailiwi ni moto hivyo
watakaobainika watashughulikiwa “Alisema.
Hata
hivyo alisema kwamba wilaya hiyo imepokea milioni 362.5 kutoka
Serikalini kwa ajili ya ukamilishaji na umaliziaji wa vyumba vya
madarasa 29 vya shule ya msingi wilayani humo.
Fedha
hizo zilitolewa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt
John Magufuli ambaye amepania kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo
kwa vikwazo vya aina yoyote ile.
Alisema
kwamba bado ujenzi unaendelea kwa sehemu mbalimbali na haitafikia mwezi
Agosti majengo hayo yatakuwa yamekamilika na hivyo kuondokana na
changamoto zilizopo.
“Lakini
pia niwapongeze Asasi ya Tree of hope kwa maana maeneo mradi huo
umefanya kazi kuna mabadiliko makubwa ya uwazi na uwajibika lakini pia
hata utoro umepungua kwa asilimia kubwa hivyo mradi huo umekuwa chachu
kubwa sana kwa jamii “Alisema.
Awali
akizungumza wakati wa mkutano huo wa wadau Mratibu wa Mradi wa
Kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika
kuboresha elimu kwenye vijiji nane Goodluck Malilo alisema kwamba mradi
huo rasmi kutekelzwa na Asasi ya Tree of hope katika wilaya hiyo mwezi
Agosti mwaka 2017 hdi Mwezi Julai 2018.
Alisema
kwamba mradi huo ulikuwa ukitekelezwa kwenye vijiji vinne vya
Halmashauri ya Handeni ambazo ni Michungwani (Kata ya Segera),
Kwedizinga (Kata ya Kwedizinga), Kabuku Nje (Kata ya Kabuku) na Komsanga
(kata ya Mgambo) chini ya ufadhili wa shirika la Foundation for Civil
Society.
Malilo
alisema baada ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza na
kuonekana mafanikio makubwa asasi hiyo iliongezewa muda wa ufadhili kwa
kipindi cha miezi mitano kuanzia Novemba mwaka 2018 hadi mwezi Machi
2019 ili kuendeleza kutatua changamoto za elimu katika vijiji hivyo.
Alisema
kutokana na mafanikio ya mradi huo kuwa endelevu na yenye tija katika
sekta ya elimu waliomba ufadhili kutoka Shirika la Foundation for Civil
Society ili kutanua wigo wa maeneo ya utekelezaji kutoka vijiji vinne
had inane ambapo walikubaliwa huku wakiongeza vijiji vya Mjani Mapana
(Kabuku ndani),Hoza(Komkonga),Kitumbi (Kitumbi) na Mkata Mashariki
(Mkata).
Hata
hivyo alisema kwamba mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi nane
kuanzia mwezi Julai 2019 hadi February 2020 huku akieleza shughuli za
mradi zitakazotekelezwa katika vipindi viwili vya miezi minne minne .
Alisema
shughuli hizo ni pamoja na mikutano ya wadau wa elimu,uundaji wa kamati
za wananchi za uhamasishaji na ufuatiliaji uwajibikaji ,mafunzo ya
utawala bora,midahalo ya wadau wa elimu,uhamasishaji uwajibikaji jamii
na mamlaka husika katika kuboresha elimu ikiwemo utengenezaji na
usambazaji wa vipeperushi vya uelimishaji ikifuatiwa na ziara za
ufuatiliaji na tathimini katika maeneo ya mradi.
No comments :
Post a Comment