Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard
Kalemani (watatu kushoto), akiwa na Naibu Waziri wa Nishati ambaye pia
ni Mbunge wa Kigamboni, Mhe. Dkt.Faustin Ndungulile (wapili kushoto),
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Ruth Msafiri na viongozi wengine,
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa REA III kwa maeneo yaliyo
pembezoni mwa miji,. Uzinduzi huo ulifanyika Kigamboni Agosti 2, 2019.
Dkt.
Kalemani akizindua mradi huo huku akiwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt.
Faustin Ndungulile (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Ruth
Msafiri.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akihutubia wananchi wakati wa uzinduzi huo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akihutubia wananchi wakati wa uzinduzi huo.
Dkt. Kalemani (kulia), akipungia mkono
wananchi huku akionbgozana na Naibu Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge
wa Kigamboni, Dkt. Faustin Ndungulile (katikati).
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Mhe. Ruth Msafiri akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
Dkt. Kalemani akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Ruth Msafiri
Alisema malengo ya serikali ni kuhakikisha wananchi
wote mijini na vijijini wanapelekewa umeme ifikapo mwaka 2021/2022 ili waweze
kunufaika kupitia huduma hiyo ya nishati katika kujiletea maendeleo.
NA
K-VIS BLOG
WAZIRI
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amezindua Mradi wa REA awamu ya III kwa Wilaya zilizo pembezoni mwa Miji ikiwemo Wilaya
ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi
huo umefanyika Agosti 2, 2019 huko Kigamboni ambapo Mhe. Dkt. Kalemani
amemuagiza mkandarasi kumaliza kazi kwa wakati kama ambavyo mkataba
unavyoeleza.
Dkt. Kalemani amesema shunghuli za kiuchumi zimeongezeka sana pamoja
na ongezeko la idadi ya Watu wenye uhitaji wa kuunganishiwa umeme nayo pi aim eongezeka
kwa hivyo nitoe rai kwa mkandarasi kufanya kazi kwa kasi ili mradi huu
ukamilike na wananchi wetu wapate umeme.” Alisisitiza Dkt. Kalemani wakati
akihutubia kwenye hafla hiyo.









No comments :
Post a Comment