Sunday, August 4, 2019

WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA BoT, MAAFISA WASEMA WENGI WANAPENDA KUELIMISHWA KUHUSU NOTI BANDIA NA MAHITAJI YA CHENJI


Maafisa wa BoT wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la BoTviweanja vya Nyakabindi Simiyu leo Agosti 3, 2019.
Wananchi wakitazama noti za Benki Kuu ya Tanzania BoT, ili kubaini zilizo halali na zile za bandia, walipotembelea banda la BoT kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi, Simiyu leo Agosti 3, 2019.
Maafisa wa BoT wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la BoTviweanja vya Nyakabindi Simiyu leo Agosti 3, 2019.
Maafisa wa BoT wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la BoTviweanja vya Nyakabindi Simiyu leo Agosti 3, 2019.
Wananchi wakitazama noti ili kujifunza namna ya kubaini zilizo halali na zile za bandia (Feki)  walipotembelea banda la BoT viwanja vya Nyakabindi Simiyu leo Agosti 3, 2019.

Maafisa wa BoT wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la BoTviweanja vya Nyakabindi Simiyu leo Agosti 3, 2019.NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
WANANCHI wengi wamekuwa wakimiminika kwenye banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Banda la BoT limekuwa kivutio kwa watu wengi hususan wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa jirani ambapo wamekuwa wakifika kwenye banda hilo kupata taarifa kuhusu namna ya kugundua noti bandia, kubadilisha fedha zilizochakaa na kupatiwa noti mpya, lakini pia kuelimishwa kuhusu majukumu yab Benki Kuu.
Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanafanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu Agosti 1, 2019 na yatafikia kilele Agosti 8, 2019.
Maonesho yamebeba kauli mbiu isemayo "Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa nchi.".

No comments :

Post a Comment