| Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akimkabidhi kadi ya CCM, aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wa kata hiyo, Hawa Mdamu aliyehamia CCM. |
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki
Kingu akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Irisya
wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Diwani wa Kata ya Irisya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ali Mwanga akizungumza.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akilakiwa baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Irisya, Ibrahim Kivandu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata hiyo, Juma Nkungu akizungumza.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akiserebuka katika mkutano huo.
Wakina mama wa Kijiji cha Kitandaa wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mbunge wa Singida
Magharibi, Elibariki Kingu, akimkabidhi kadi ya CCM, aliyekuwa Katibu wa
Umoja wa Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wa kata hiyo,
Fatuma Makuku aliyehamia CCM.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WANANCHI wa Kata ya Irisya iliyopo
wilayani Ikungi mkoani Singida wamefurahia kupata maji ya bomba ambayo
hawakuwahi kuyapata tangu nchi hii ipate uhuru.
Kupatikana kwa maji hayo kumetokana na
jitihada za Mbunge wao wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu
za kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo kwa kushirikiana na Serikali.
Akizungumza jana katika mkutano wa
hadhara aliouandaa mbunge huyo Diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ali Mwanga alisema
ilikuwa ni chereko na nderemo kwa wananchi wa Kata hiyo na vitongoji vya
jirani baada ya kupata maji kwa mara ya kwanza kwenye kata hiyo.
Alisema juzi ilikuwa ndio siku ya
kufanya majaribio ya kutoa maji baada ya kupelekewa mradi mkubwa wa maji
na Serikali kupitia mbunge wao.
Alisema baada ya kufunguliwa maji hayo
wananchi wa kata hiyo waliweza kuteka maji hayo kwa zaidi ya masaa
matano huku wengine wakitoka umbali wa kilomita nne hadi tano jambo
ambalo lilionesha furaha kwao.
Alisema kuwa bomba hilo lina uwezo wa
kutoa maji lita 18,600 kwa saa ambapo ni sawa na pipa 740 na kuwa kata
hiyo itajitosheleza kwa maji na ziada itakwenda vitongoji vingine vya
jirani.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wa Kata hiyo, Juma Nkungu alisema tangu wamepata Uhuru hakuna mbunge
ambaye aliwahi kuwafikia wananchi kwa kuwapelekea maendeleo kwa kiasi
hicho kama Kingu.
"Kwa kusema ukweli Kingu amegusa kila
kitongoji cha jimbo letu katika kuleta maendeleo tunasema hatumtaki
mbunge mwingine zaidi yake kwanza anamsaidia sana Rais wetu Dkt.John
Magufuli na tunamuhakikishia katika chaguzi zinazo kuja tutawapa kura za
kutosha kuanzia Rais, Mbunge na Diwani wetu Ali Mwanga" alisema
Nkungu.
Akihutubia katika mkutano huo Kingu
alisema katika kipindi cha miaka minne tangu wachaguliwe serikali ya
awamu ya tano imefanya kazi kubwa ya maendeleo katika nchi hii baada ya
Rais Dkt.John Magufuli kudhibiti fedha zilizokuwa zikitumika hovyo na
kuziba mianya ya wizi na fedha hizo kuzielekeza katika shughuli za
maendeleo kama vile ununuzi wa ndege, ujenzi wa vituo vya afya,
barabara, umeme, reli na miradi mingine.
No comments :
Post a Comment