Sunday, August 4, 2019

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) YASISITIZA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUKATA BIMA YA KILIMO

 Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini, Bw. Eliezer Rweikiza akitoa ufafanuzi kuhusiana na Bima ya kilimo katika maonesho ya 26 ya Nanenane Kanda ya kaskazini kwenye viwanja vya Themi, Njiro jijini Arusha.
 Paulo Makanja ni Mwanasheria Mwandamizi kutoka TIRA:amesisitiza wakulima wanaodai malipo ya Bima wafike banda la TIRA kwaajili ya msaada zaidi
 Meneja wa TIRA kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akisisitiza kwajambo mteja kama anavyoonekana katika picha,kushoto kwake ni Paulo Makanja ni Mwanasheria Mwandamizi kutoka TIRA 

Na Vero Ignatus, Arusha
Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA imepitisha na kutoa mwongozo wa Bima ya kilimo ikiwa na maana ya kusisitiza wananchi ambao wanajihusisha na
kilimo kwenda  katika maonyesho ya 88 ili waweze kupatiwa huduma ili kukinga kilimo chao na mifugo yao. Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Bw. Eliezer Rweikiza  amesema. 
Alisema ziko faida nyingi za kukata bima ya kilimo kwani  mkulima anapokata bima ya kilimo inamkinga dhidi ya majanga  ya kilimo anapopata hasara kutokana na majanga hayo anafidiwa na kampuni husika ya bima. 
Bw. Eliezer amesema hivi karibuni  Mamlaka ilieendesha mafunzo  kwenye vikundi takribani 50 vinavyojumuisha VICOBA, SACOS, AMCOS, pamoja na wajasiriyamali juu ya umuhimu w abima kwenye shughuli zao hususan kilimo.

 Ameainisha vijiji ambavyo wametoa elimu kwa ujumla kuwa ni pamoja na Tanga mjini vikundi 10,  Wilaya ya Muheza 12, Korogwe 11, Babati 6, na Hanang 8.

Rweikiza mesema huduma za bima  zimekuwa zikutolewa zaidi ya miaka mitano nyuma ila kwa sasa zinakuwa na vitu ambavyo vimeboreshwa zaidi kwani zipo huduma hadi kwa wakulima wadogo
"Hivyo basi bima ni muhimu sana kwa wote wanaolima au kufanya shughuli za ufugaji na haijalishi kilimo kikubwa au kilimo kidogo wote wanaweza kupatwa na majanga na kwakweli tunawasihi sana wakulima wa  Kanda hii kukata bima ya Kilimo na Mifugo ili kujihakikishia usalama wa kilimo chao na mifugo." Alisisitiza. 

No comments :

Post a Comment