Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akivikwa shada la maua
baada ya kuwasili Kijiji cha Kitandaa kwa ajili ya kufanya mkutano wa
hadhara wilayani Ikungi mkoani Singida jana. Mbunge Kingu alifanya
mikutano miwili katika kijiji hicho na makao makuu ya Kata ya Mtunduru.
Wakina mama wa Kijiji cha Kitandaa wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea Kijiji cha Kitandaa.
Mbunge Kingu akisalimiana na wazee wa Kata ya Mtunduru baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya mkutano.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzì (UVCCM) wilaya ya Ikungi, Jafari Dude akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Ikungi,
Himid Tweve, akiimbisha wimbo wa viongozi wamechachamaa.
Diwani wa Kata ya Mtunduru Ramadhan Mpakii akizungumza.
Wanawake wa Kata ya Mtunduru wakiwa kwenye mkutano huo.
Mbunge Kingu akihutubia kwenye mkutano huo wa Kata ya Mtunduru.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Novatus Kibaji akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Singida
DIWANI
wa Kata ya Mtunduru katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani
Singida, Ramadhani Mpakii amesema jitihada zinazofanywa na Mbunge wao
Elibariki Kingu za kuwapelekea miradi ya maendeleo zinapaswa kuungwa
mkono na kila mpenda maendeleo wa Jimbo la Singida Magharibi.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti jana kwenye mikutano ya hadhara aliyoandaa mbunge
huyo katika vijiji vya Kitandaa na Mtunduru Mpakii alisema haijawahi
kutokea tangu vianzishwe vijiji hivyo kwa kupata maendeleo makubwa
katika kipindi cha miaka minne tangu mbunge huyo aingie madarakani.
"
Mbunge huyu hana wa kumlinganisha naye ni msikivu na amejitahidi sana
kutuletea maendeleo katika Kata yetu ebu tumuache aendelee kututumikia
kwa kipindi kingine kwanza umri wake bado ni mdogo " alisema Mpakii.
Alisema
katika kata hiyo ameweza kujenga shule, zahanati, na sasa amewaletea
mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh.milioni 405 ambao utasambaza
maji kwenye vijiji vyote vya kata hiyo.
Mpakii
aliongeza kuwa tangu miaka 50 iliyopita hakujawahi kutokea Mbunge kama
Kingu kwani kazi iliyofanywa na Rais Dkt.John Magufuli na Mbunge huyo ya
kuwapelekea miradi hiyo itawarahisishia upatikanaji wa kupata kura
nyingi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mtaa na uchaguzi mkuu
utakaofanyika mwakani.
"
Kwa kazi hii kubwa iliyofanyika hatuna wasiwasi CCM itapata ushindi wa
kishindo ambao haujawahi kupatikana katika uchaguzi wowote tuliowahi
kuufanya" alisema Mpakii.
Akizungumza
katika mkutano huo Kingu aliwashukuru wananchi na kuwaambia maendeleo
hayo wanayapata baada ya Rais John Magufuli kuwabana mafisadi na
matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kwa wananchi
wanyonge kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.
Alisema
haijawahi kutokea kwa kipindi chote kilicho pita ndani ya jimbo hilo
kufanyika kwa miradi mingi kiasi hicho ikiwemo miradi mikubwa ya maji 24
huku mchakato wa kupata umeme wa REA ukiendelea na kuwa amepata fedha
zaidi ya sh. milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika
Shule ya Sekondari ya Mtunduru.
Wakati
huo huo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi, Novatus
Kibaji, ametoa onyo kwa wanachama wa chama hicho kuanza kujipenyeza
kwenye majimbo ili kuwania nafasi za ubunge na udiwani wakati majimbo
hayo yakiwa na wawakilishi.
No comments :
Post a Comment