Na; Mwandishi Wetu
Wawekezaji
wameshauriwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za kazi zilizopo nchini
ili kuongeza ufanisi na tija katika sekta ya kazi.
Akizungumza
mara baada ya kuwasili katika shamba hilo alieleza kuwa wawekezaji
wakiwa kama waajiri lazima wahakikishe wanafuata sheria za kazi katika
maeneo yao ya uzalishaji kwa kuzingatia masuala ya msingi ya wafanyakazi
ili waweze kuzalisha kwa tija na kuwahamasisha kufanya kazi zao kwa
juhudi.
“Serikali
ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli imeendelea kuboresha mazingira ya biashara ambayo yamekua
yakivutia zaidi wawekezaji, hivyo sera nzuri zilizopo nchini zimekuwa
chachu kwa wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu,” alisema Mhagama
Alieleza
pia, endapo wawekezaji watafuata miongozo ya kisheria katika masuala ya
kazi na ajira yatawarahisishia utendaji wao wa kazi.
Akitolea
mfano kuhusu masuala ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi, likizo ya uzazi
kwa wanawake, uwazi wa mikataba ya ajira, uhuru wa mfanyakazi kujiunga
na chama cha wafanyakazi, haki ya kupatiwa vitendea kazi na maslahi ya
wafanyakazi ni baadhi ya vitu vya msingi ambavyo mwekezaji inabidi atoe
kwa mfanyakazi wake kwa kuzingatia taratibu na sheria.
Hata
hivyo aliongezea kuwa ushirikiano na vyama vya wafanyakazi ni jambo la
muhimu kwa kuwa vimekuwa vikitetea masuala ya wafanyakazi ambayo
yamekuwa yakijitokeza katika maeneo yao ya kazi, pamoja na kuwa na
mkataba wa hali bora za wafanyakazi baina ya mwajiri na mwajiriwa.
Sambamba
na hilo Mheshimiwa Mhagama alitoa maagizo kwa timu ya wataalamu ambao
aliambatana nayo kutoka Idara ya Kazi, Wakala wa Usalama na Afya mahala
pa Kazi (OSHA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii (NSSF), Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Tume ya Usuluhisi na Uamuzi pamoja na
Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi kuendelea kutoa elimu kwa umma hususan
wafanyakazi ili watambue sheria za kazi na namna taasisi hizo zinaweza
kuwasaidia katika kupata ufumbuzi wa masuala yao ya kazi.
Aidha,
Waziri Mhagama alitoa pongezi vilevile kwa wawekezaji wa Shamba la
Katani la China State Farms kwa kuwajali wafanyakazi wao ikiwa na
kuwajengea nyumba bora za kuishi wafanyakazi wao.
“Nimpongeze
mwekezaji kwa kuona umuhimu wa kuwajengea makazi wafanyakazi ambayo
yatamaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa nyumba na umbali ambao
wafanyakazi wamekua wakitumia kwenda kazini,” alisema Mhagama
Pia,
alitumi muda huo kuwahamasisha wafanyakazi kutumia muda wao wa ziada
katika mashamba yao binafsi na kujiunga kwenye mashamba ya ushirika
yatakayo wawezesha kupata soko la uhakika kutoka kwa mwekezaji huyo ili
waweze kuimarika kiuchumi.
Naye,
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi alisema kuwa Sheria za kazi
zimekuwa zikitoa mwongozo mzuri kwa wawekezaji katika kuimarisha
shughuli zao za uzalishaji, kutoa ajira pamoja na kuchangia kwenye
mapato ya nchi.
Kwa
upande wake, Meneja wa Kiwanda hicho Bw. Majuto Chitema alitoa pongezi
zake kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusifu juhudi
alizonazo katika kuboresha na kuwajengea mazingira wezeshi wawekezaji,
kwani serikali yake imeweza mstari wa mbele kuweka sera, miongozo,
kanuni na sheria ambazo zimekuwa haziwabani wawekezaji.
Miongoni
mwa Wafanyakazi wa China Estate Farms Bw. Azory Andrea alisema kuwa
Serikali iendelee kuangalia namna ya kuwa kuwasimamia wawekezaji waliopo
nchini ili waweze kutekeleza wajibu wao kwa wafanyakazi kwa mujibu wa
sheria za kazi.
Kabla
ya ziara hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
aliwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata
taarifa ya maeneo aliyoandaliwa kutembelea katika ziara yake mkoani
hapo.
No comments :
Post a Comment