
Naibu Msajili wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe. Kelvini Mhina akitoa elimu juu ya Mahakama
Inayotembea kwa wananchi waliofika Mahakamani hapo kupatiwa huduma
mbalimbali. (Picha na Aziza Muhali)

Baadhi ya wananchi waliofika
kupatiwa huduma za kimahakama katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakisikiliza maelezo juu ya utendaji kazi wa Mahakama Inayotembea.
Na Aziza Muhali
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
iliyopo jijini Dar es Salaam leo imetoa elimu juu ya
Mahakama
Inayotembea kwa wananchi ili waweze kuifahamau na kupata huduma
zinazotolewa na Mahakama hiyo.
Akizungumza na wananchi ambao
walifika katika Mahakama hiyo ili kupata huduma mbalimbali, wakati wa
utoaji wa elimu kwa umma, Naibu Msajili wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Mhe. Kelvin Mhina, amewataka wananchi kufikisha ujumbe wa
Mahakama Inayotembea, kwa wananchi wengine ili waweze kufahamu jinsi
Mahakama hiyo inavyofanya kazi.
“Mahakama hii ni Mahakama
inayotembea na iliyokamilika inayowafikia wananchi katika makazi yao
lengo likiwa ni kuboresha na kusogeza huduma za Mahakama karibu na
wananchi, “alisema Mhe.Mhina.
Aliongeza kuwa maeneo
yatakayohudumiwa na mahakama hiyo ni wakazi wa Bunju A ambapo Mahakama
hiyo itatoa huduma katika viwanja vya Ofisi ya Serikali za Mitaa,
Kibamba, Viwanja vya Ofisi ya Wilaya ya Kinondoni, Chanika, pembeni ya
Kituo kipya cha Polisi Chanika, Buza, eneo la kituo cha Mabasi Buza.
Kwa upande wake Karani Mkuu
Kitengo cha Jinai, Imakulata Konala ambaye pia ni Msaidizi Mkuu wa
Kumbukumbu kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amewataka wananchi
hao kuepuka kupewa huduma na watu wasiojulikana kisheria ,bali wawatumie
watumishi wa Mahakama ambao huvaa vitambulisho vya kazi.
No comments :
Post a Comment