
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu
Nyerere mabadiliko ya Tabia ya Nchi, Prof.Pius Yanda akizungumza na
Wanahabari katika mkutano uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.
***************
NA EMMANUEL MBATILO
Watafiti na wanasayansi takribani
300 kutoka bara la Afrika na nje ya Afrika wanatarajia kushiriki
Kongamano la kimataifa litakalojadili mjadala utakaojikita katika
kuainisha jinsi
matokeo ya tafiti yanaweza kusaidia katika jitihada za
kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kongamano hilo linatarajia
kufanyika katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam Oktoba 8 na 10 mwaka huu.
Akizungumza na Wanahabari Jijini
Dar es Salaam mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere mabadiliko ya
Tabia ya Nchi, Prof.Pius Yanda amesema kuwa kongamano hilo litatoa
nafasi kwa wanasayansi kujadili matokeo ya tafiti mbalimbali katika
maswala ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Aidha Prof.Yanda amesema kuwa
wanawaalika watafiti,wana taaluma na wale wote wanaoshiriki katika
shughuli za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi kwa njia moja au
nyingine pamoja na wale wote watakaoopenda kushiriki.
“Kongamano hilo litajikita katika
maeneo ya Usimamizi wa maliasili na mifumo yake ya ki-ekologia katika
kipindi chenye changamoto ya mabadiloko ya Tabia Nchi, Mabadiliko ya
Tabia nchi na Usalama wa Chakula pamoja na nyingine ya Ubunifu wa
Teknolojia, maadili katika usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya Tabia
Nchi”. Amesema Prof.Yanda.
No comments :
Post a Comment