Afisa
uwajibikaji kwa jamii wa Tigo , Halima Okash. (kushoto) akimkabidhi
mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu , Sylvia Lyimo
(wa pili kulia) moja wapo ya kompyuta 10 zilizotolewa na kampuni ya Tigo
katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam (wa pili
kushoto ni Diwani wa kata ya Kisutu Kheri Mohamed Kessy.
Afisa
uwajibikaji kwa jamii wa Tigo , Halima Okash. Akionyeshwa na wanafunzi
wa shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu jijini Dar es Salaam,jinsi ya
kutumia kompyuta mara baada ya kukabidhi msaada wa kompyuta 10
zilizotolewa na kampuni ya Tigo, kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,
Sylvia Lyimo.
Baadhi ya wanafunzi wakifurahia kutumia kompyuta muda mfupi baada ya
kukabidhiwa masada wa komuta 10 kutoka Kampuni ya Tigo.
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni inayoongoza katika maisha ya kidigitali nchini Tanzania ya Tigo,
leo imetoa msaada wa... kompyuta 10 shule ya sekondari ya wasichana
Kisutu, pamoja na kuwaunganisha na intaneti ya bure kwa ajili ya
kuwawezesha wanafunzi kupata elimu kupitia teknolojia ya kisasa.
Msaada huo umeenda sambamba na uzinduzi wa kituo cha kupata elimu
kutumia njia za kisasa za kidigitali kwa shule za Sekondari mkoani Dar
es Salaam. Wanafunzi watawezeshwa kupata fursa ya kutumia kituo hicho
kupata maarifa ya matumizi ya kompyuta na TEHAMA.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Afisa Uwajibikaji kwa
Jamii kutoka Tigo, Halima Okash alisema, “Msaada huu tuliotoa leo
kusaidia shule ni moja ya ufanikishaji wa mkakati wetu wa kuwezesha
matumizi ya kidigitali ambapo shule zikiwezeshwa kutumia teknolojia
kufundisha wanafunzi, wataweza kupata maarifa sambamba na kunufaika kwa
kutoachwa nyuma katika mapinduzi ya kiteknolijia ya Kisasa matumizi ya
TEHAMA yanayoendelea duniani”.
Alisema kutokana na ongezeko la matumizi ya kompyuta nchini Tanzania,
sio shule zote zinauwezo wa kutoa elimu ya matumizi ya teknolojia hii.
Moja ya changamoto inayowakabili wanafunzi wa shule za sekondari nchini
ni kukosekana kwa nyenzo za kuwawezesha kupata elimu inayohusiana na
matumizi ya teknolojia za kisasa.
“Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kisutu, sasa wanaweza
kupata mafunzo ya matumizi ya kompyuta katika mitaala ya masomo yao.
Elimu ya TEHAMA inaweza kuleta mabadiliko haraka katika sekta ya elimu,
ambapo wanafunzi wanaweza kupata maarifa kutoka kwenye mitandao na
tovuti mbalimbali za kielimu, kujifunza mambo mengi na kupata ujuzi
unaotakiwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi.” alisema.
Aliongeza kusema “Uzinduzi wa kituo hiki cha kutoa elimu kupitia TEHAMA,
unadhihirisha dhamira ya kampuni ya Tigo, kufanya uwekezaji katika
miradi ya kusaidia jamii hususani kuleta mapinduzi ya sekta ya elimu
kuwa ya kisasa na ya kidigitali, sambamba na kufanya shule hii kuvutia
wanafunzi wengi wa shule jirani wenye kiu ya kupata elimu ya matumizi ya
kompyuta na TEHAMA.
Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Kisutu, Mh. Khery Kessy, ambaye
alikuwa ni mgeni rasmi aliipongeza kampuni ya Tigo, kwa juhudi zake za
kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha mazingira ya kusomea
nchini.
“Nawashukuru Tigo kwa msaada huu, kwa kuwa utawezesha wanafunzi kupata
maarifa ya elimu kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa mapema wakiwa
bado wako katika madarasa ya chini katika safari yao ndefu ya kutafuta
elimu. Ujuzi watakaopata kupitia kompyuta hizi utawawezesha kwenda na
wakati wa kisasa na kuweza kuwa na sifa ya kupata ajira.” alisisitiza.
Mmoja wa wahitimu wa programu ya Tigo inayojulikana kama Change makers,
ya mwaka 2014, amejitolea kushiriki kuwafundisha wanafunzi wa shule hiyo
na kushirikisha wanafunzi kutoka shule nyingine za sekondari, ufadhili
huu wa kampuni ya Tigo utawezesha wanafunzi kushiriki na kuwavutia
kutaka kujua matumizi ya TEHAMA katika kufanikisha ndoto zao katika
masomo yao.
Katika miaka ya karibuni, kampuni ya Tigo imetoa msaada wa kompyuta 77
katika shule na vyuo vya Serikali, ikiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma, Shule
ya Sekondari ya Jangwani, iliyopo jijini Dar es Salaam, shule 3 za
sekondari mkoani Mtwara na shule moja ya msingi mkoani Tanga.
No comments :
Post a Comment