Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Simiyu, Bw.Mawazo Ngeraniza (kulia), akitoa elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii kwa wanachama wa PSSSF waliotembeela banda la Mfuko huo kwenye maonesho hayo. |
Meneja Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi.
Rehema Mkamba akimfafanualia jambo mwanachama wa Mfuko alipotembelea
banda la Mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Rehema Mkamba akimfafanualia jambo mwanachama wa Mfuko alipotembelea banda la Mfuko huo.
Timu ya PSSSF iliyoweka kambi kwenye banda namba 37 la Mfuko huo mkabala na BoT kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mkoa wa Simiyu, umesema
utatoa huduma bora na zenye viwango katika kipindi chote cha Maonesho ya...
Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji
wa Bariadi mkoani humo.
Kaimu
Meneja wa Mfuko huo Mkoa wa Simiyu, Bw.Mawazo Ngeraniza amesema leo Agosti 2,
2019 kuwa timu ya wafanyakazi wa PSSF imejipanga tayari kutoa huduma hizo
kwenye banda namba 37 la PSSSF lililo mkabala na Banda la Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), na kuwaalika wanachama wote na wananchi kwa ujumla kufika kwenye banda
hilo ili kuhudumiwa kwa kasi na viwango.
“Sisi
tunaamini kuwa jukwaa hili la maonesho ya nanenae hapa Nyakabindi, limewaleta
pamoja wanachama wetu wengi tu, kama ujuavyo Mfuko wetu unawahudumia watumishi
wa umma, na hapa kuna watumishi wengi kutoka taasisi za umma wanashiriki katika
maonesho haya kutoka sehemu mbalimbali za nchi yeu ni fursa nzuri kwetu
kuwahudumia kwa ukaribu na kwa haraka tunachoweza kusema kila wapatapo muda
watembelee banda letu nasi tutawahudumia.” Alisema na kufafanua.
Huduma
tunazotoa kwenye banda letu ni sawa kabisa na zile zinazotolewa kwenye ofisi zetu
zilizoenea mikoa yote ya Tanzania bara ikiwemo Zanzibar, hivyo basi ukifika
kwenye banda letu utapata taarifa za Pensheni ya Uzeeni,
taarifa za Mafao ya kukosa Ajira, taarifa za Mafao ya Uzazi, taarifa za Dhamana
ya Mikopo ya Nyumba, taarifa za Uwekezaji lakini pia wastaafu watapata fursa ya
kuhakiki taarifa zao kwani zoezi la uhakiki ni endelevu.” Alifafanua Bw. Ngeraniza.
"Mfuko wa PSSSF umeundwa baada ya kuunganishwa kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii
ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF na kwa sababu hiyo bado ni mpya na wanachama
wanahitaji kuelimishwa kuhusu majukumu mapya ya Mfuko huo kwa wanachama ambao
ni watumishi wa Umma.", alisema
Maonesho
ya Nanenane hapa yamefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muunganomwa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan Alhamisi Agosti 1, 2019
na yatafikia kilele Agosti 8, 2019.
Kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni "Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.".
No comments :
Post a Comment