
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda akizungumza na
wahitimu wa mafunzo ya wiki 3 ya usalama Mahali pa kazi na kuwahimiza
kutumia maarifa hayo ili kuleta tija katika uzalishaji
************
NA EMMANUEL MBATILO
WAKALA wa usalama na Afya Mahali
pa kazi (OSHA) wafanyakazi wanahitaji ongezeko la mafunzo ya mahali pa
kazi kwa kiwango Cha hali ya juu nchini.
Akizungumza na waandishi wahabari
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA)
Khadija Mwenda alipokua akihitimisha mafunzo ya kozi ya Taifa ya usalama
na Afya Mahali pa kazi (National occupational safety and Health
course-) amesema kozi hiyo imetolewa kwa wiki tatu mfululizo katika
ofisi za (OSHA) Kinondoni jijini Dar es salaam.
Aidha,Mwenda amefafanua kuwa jumla
ya washiriki 107 kutoka taasisi, makampuni,mashirika na watu binafsi
kutoka mikoa mbalimbali kote nchini.
“Kozi hii tulikua tunaitoa mara
kwa mwaka lakini kutokana na uhitaji wa mafunzo hayo kuongezeka
tumelazimika kutoa kwa awamu nne kwa mwaka,”
Mwenda aliongezea kuwa kimsingi
kumekua na mwamko mkubwa sana miongoni mwa taasisi za umma, makampuni
binafsi na mtu mmoja mmoja ambao wanafika ofisi za osha kupata mafunzo
hayo muhimu kwa ajili ya kuandaa wataalam wa kusimamia masuala ya
usalama na Afya katika sehemu za kazi.
Pia ametoa wito kwa wahitimu wa
mafunzo hayo kuzingatia na kutumia maarifa waliopata katika kuleta
mabadiliko chanya kwenye maeneo ya kazi hususan katika kuboresha
mazingira ya kazi ili kuongeza tija katika uzalishaji.Kwa
upande wake mshiriki wa mafunzo hayo amesema ni muhimu sana kwa
watanzania wote kuimarisha masuala ya afya na usalama katika maeneo ya
kazi.
No comments :
Post a Comment