
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za
Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto
Dkt. Timothy Wonanji (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila mara baada ya kutembelea
hospitalini hapo.

Mhandisi wa Hospitali ya
Mloganzila, Happymark John (wa kwanza kushoto) akielezea jinsi tanki la
kuhifadhi maji linavyofanya kazi.

Mhandisi Akaniwa Msengi (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kuhusu mtambo wa liquid oxygen.

Mhandisi Msengi akiwaelezea
wataalam wa Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar jinsi mtambo wa oxygen
mbadala unavyofanya kazi. Ujumbe wa wataalam hao umetembelea Hospitali
ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kujifunza matumizi ya oxygen kwa
wagonjwa.
……………………….
Dar es salaam
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imesema itaendelea kushirikiana na
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila katika kuhakikisha inatatua
changamoto zilizopo
ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za fya.
Kauli hiyo nimetolewa na
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Timothy
Wonanji mara baada ya kutembelea Hospitali ya Mloganzila ili kuangalia
utoaji wa huduma, miundominu na changamoto zilizopo.
“Nawapongeza kwa utendaji wenu wa
kazi nahidi tutaendelea kushirikiana katika kuhakikisha Hospitali ya
Mloganzila inafikia malengo yake na wananchi wanaendelea kupata huduma
bora’’amesema Dkt. Wonanji.
Katika hatua nyingine, Ujumbe wa
wataalam kutoka Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar umetembelea Hospitali
ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kujifunza matumizi ya oxygen kwa
wagonjwa.
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya
Mnazi mmoja Zanzibar, Haji Nyonje Tandu amesema ujumbe huo umehusisha
viongozi wa ngazi mbalimbali kwa lengo kujifunza jinsi oxygen
inavyopatikana, matumizi yake kwa wagonjwa na kuona namna mitambo
inavyozalisha na kusambaza.
“Tumekuja kujifunza kwenu ili
tuendelee kuboresha utoaji huduma za afya kwa wananchi kwani hospitali
yetu ina matumizi makubwa ya oxygen ikiwa ni wastani wa mitungi 45 kwa
siku, hivyo inatupasa kuendelea kujifunza zaidi’’amesema Bw. Haji Nyonje
Tandu.
No comments :
Post a Comment