
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akijadili jambo na Kaimu Mwenyekiti
wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela Profesa
Lughano Kusiluka wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha TEHAMA.

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akimpongeza Makamu Mkuu wa Taasisi
ya Nelson Mandela Prof. Emmanuel Luoga baada ya kuzindua Kituo cha
Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya
Nelson Mandela jijini Arusha.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya
Nelson Mandela jijini Arusha.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akizungumza
na wajumbe (Hawapo pichani) walioshiriki katika uzinduzi wa Kituo cha
Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano uliofanyika katika
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako pamoja na wajumbe walioshiriki
katika uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano wakifatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa katika uzinduzi
huo katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini
Arusha.
***************
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amezindua Kituo cha umahiri cha
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Afrika Mashariki @ Centre of
Excelence for
ICT in East Afrika kilichoanzishwa katika Taasisi ya
Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST )Arusha, Tanzania.
Akizungumza katika uzinduzi huo,
Profesa. Ndalichako amesema kituo hicho kilichofadhiliwa na Serikali ya
Ujerumani kinalenga kuwajengea uwezo watanzania pamoja na wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano katika kuleta maendeleo kwa ikiwa ni pamoja na kutoa
ufadhili wa masomo ya shahada za uzamili “Masters”.
Waziri Ndalichako amesema Mwongozo wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unatambua nafasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nyanja mbalimbali yakiwemo masuala ya viwanda, uchumi na maeneo mengine akitolea mfano mifumo ya fedha inayotumia TEHAMA inavyotumika afrika mashariki.
Waziri Ndalichako amesema Mwongozo wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unatambua nafasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nyanja mbalimbali yakiwemo masuala ya viwanda, uchumi na maeneo mengine akitolea mfano mifumo ya fedha inayotumia TEHAMA inavyotumika afrika mashariki.
“Teknolojia na ubunifu kwa ujumla
ni nyenzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na
tunapozungumzia uchumi wa viwanda hatuwezi kufanikiwa kama hatutatoa
kipaumbele katika teknolojia, lakini pia kama hatuta kuwa makini katika
kutumia tafiti na uvumbuzi katika juhudi mbalimbali za maendeleo”
amesisitiza Prof. Ndalichako
Waziri Ndalichako amewashukuru
wafadhili wa kituo hicho serikali ya Ujemani ambao tayari wametoa kiasi
cha Euro Milioni 1.384 ambayo ni takriban Shilingi Bilioni 3.5 za
Kitanzania kati ya Euro Milioni 4 thamani ya mradi mzima utakaotekelezwa
kwa miaka minne hadi 2021. Aidha amewashukuru washirika wote wa kituo
hicho na kuwataka wanafunzi waliochaguliwa kuanza masomo katika kituo
cha CENIT@ EA kutumia fursa hiyo vizuri kwa kusoma kwa bidii na
kuonyesha vipaji vyao ili waweze kupata ujuzi katika fani
ambaowataitumia katika kuleta maendeleo katika nchi wanazotoka.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza katika uzinduzi
huo, ameishukuru Taasisi ya NM- AIST kwa kuendelea kushirikiana na
Wilaya ya Arumeru katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwa kuanzisha
Kituo cha Umahiri cha TEHAMA. Wakati huohuo ameishauri taasisi ya
Nelson Mandela kuhakikisha kituo hicho hakiwi cha wanawataalama pekee
bali pia huduma zake zisaidie wananchi hasa wakulima katika kuongeza
tija katika kilimo na mazao na kusaidia kutoa mbinu bora za kilimo
kupitia tafiti zitakazokuwa zikifanyika.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza wa taasisi hiyo, Profesa Lughano
Kusiluka amesema kituo hicho ni cha Jumuiya ya Afrika Mashariki ambacho
kitakuwa kikifundisha wanafunzi katika ngazi za shahada ya umahiri
katika teknolojia ya mambo simu , hasa masuala ya usalama wa matumizi ya
simu na mawasiliano. Amesema kwa sasa kimeanza na wanafunzi 27 kutoka
nchi za Jumuiya ya Afrika Masahariki ambapo Tanzania imetoa wanafunzi 10
kati ya hao.
Naye Meneja Mradi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka giZ Simon Hochstein,
amesema serikali ya ujerumani itaendelea kufadhili miradi mbalimbali
katika Elimu ya Juu na kuwata wataalamu kuandaa maandiko ya miradi ili
kupata fedha kama ilivyokuwa katika mradi wa Kituo hicho cha Umahiri.
No comments :
Post a Comment