Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (aliyenyoosha mikono), akizungumza
wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenye
maonesho ya nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa
Bariadi Mkoani Simiyu. Maonesho hayo yaliyobeba kaulimbiu ya "Kilimo,
Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa nchi yamefunguliwa rasmi Agosti
1, 2019 na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na yatafikia kilele
Agosti 8, 2019.
Mhe. Bashe (kulia), akisindikizwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto) na Meneja
wa Idara ya Uhusioano wa Umma na Itifaki, (BoT), Bi. Zalia Mbeo
(katikati), wakayti akitoka kwenye banda hilo baada ya kulitembeekla.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, (kulia), akisainin kitabu cha wageni huku akisikilizwa na Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT Bw. Lwaga Mwambande (kushoto).
Mhe. Bashe akiuliza maswali ili kupata
ufafanuzi kutoka kwa watumishi wa BoT alipotembelea banda la taasisi
hiyo inayosimamia masuala ya kifedha hapa nchini. (Picha:Innocent
Mmari-BoT).
No comments :
Post a Comment