Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana Senzo kulia
akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wananchi aliyefika kwenye banda lao
kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayoendelea mkoani Simiyu
NAIBU Waziri wa Viwanda Mhandisi Stella Manyanya kulia akipata maelezo
kutoka kwa maafisa wa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini
(Brela) mara baada ya kutembelea banda lao
WAKALA
wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) wamesema kwamba
wameamua kushiriki kwenye maonyesho ya kilimo ya nane nane yanayoendelea
mkoani Simiyu kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara
kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko
ya nje
Hayo
yalisemwa na Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana
Senzo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya
wakulima nane nane yanayofanyika mkoani Simiyu.
Alisema
wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo hasa ukizingatia kauli mbiu ya
mwaka huu ya nane nane ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi
wa nchi pamoja dhima ya kujenga uchumi wa viwanda.
Suzana
alisema hivyo vyote vinaenda sambamba na uwezeshaji biashara huku
akieleza lengo kubwa la mfumo ni kuhakikisha wakulima na wazalishaji wa
bidhaa nchi wanapata taarifa za mahitaji ya masoko ya nje .
“Kwa
mfano mtu anataka kusafirisha bidhaa kupeleka Ulaya ,ni rahisi sana
kupata taarifa hizi katika mfumo wa trade facilitation information
module ambapo hapo awali haikuwepo kabisa”Alisema
Alieleza kwamba wanataka wakulima,wafanyabishara wapate taarifa moja kwa moja kutoka mkoani Simiyu katika viwanja vya nane nane.
Aidha
alisema kwa mkoa huo wafugaji wengi hivyo wafugaji ni wengi hivyo
ukitaka kujua taarifa zinazohusu vibali na leseni mbalimbali katika
kupeleka mifugo yake katika soko la nje ni rahisi kwasababu taarifa zipo
ambazo zitamuwezesha kujua nini anahitaji, kwa gharama gani, itachukua
muda gani, aendee taasisi gani na iko wapi.
Aliongeza
kwamba kwa mantiki hiyo mfumo huu ni mwarobaini wa tatizo la taarifa za
kibiashara katika upatikanaji wa vibali na leseni mbalimbali nchini
huku wakiwakaribisha wananchi kufika kwenye banda lao kupata huduma
hizo.
“Lakini
pia BRELA tunatoa leseni za kundi A kama zilivyoainishwa katika sheria
Leseni za Biashara ya Mwaka 1972 na marekebisho yake…. Leseni za kundi A
ni zipi, ni zile leseni zinazotolewa kwa biashara zenye mlengo wa
kitaifa, kimataifa na zenye usimamizi maalum, biashara hizi ni kama
usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, uingizaji wa bidhaa ndani ya nchi na
biashara za usimamizi maalum kama za madini, benki na zingine kama
hizo.
Awali
akizungumza Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela suzana
Senso amesema wapo kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kuwapasha habari
wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza
kutoa huduma hata katika masoko ya nje (internatinal market) .
Hivyo
bas mkulima / mfanyabiashara akifika BRELA anapata taarifa za kibishara
zaidi katika biashara za kimataifa,asajili kampuni au jina la biashara
na anapata leseni itakayomuwezesha kusafirisha bidhaa zake nje ya nchi.
Hata
hivyo alisemwa kwamba kwa matiki hiyo sasa Brela ni one stop shop
mfanyabiashara akifika hapa anapata kila kitu kitakachomuwezesha kwenda
kufanya biashara duniani.
Naye
kwa upande wake Eliabu Rwabiyago ambaye ni Afisa kutoka Brela amesema
wakala pia ina kitengo cha kuwezesha biashara (trade facilitation
section) ambacho kimejikita katika uwezeshaji biashara.
Alisema
kwa sasa wakala huo unaandaa portal inayoitwa trade facilitation
information module , portal ambayo itajikita katika kutoa taarifa za
kibiashara nchini.
Alisema
kwasababu wafanyabiashara wengi nchini na nje ya nchi wanataka
kufanyabiashara lakini taarifa za kibiashara kwa maana ya vibali na
leseni mbalimbali zinazohitajika zinapatikanaje na kwa muda gani hivyo
kwa mtandao hayo maswali yote yamejibiwa.
Alieleza
kwamba kukamilika na kutumika kwa mfumo huu kutakuwa na faida nyingi
sana katika uwezeshaji wa biashara ikiwemo kuongeza uwazi katika utoaji
wa huduma za umma, kuiongeza ushirikiano baina ya ofisi za umma na
wafanyabiashara maana kwa kutumia mfumo watakuwa wanaweza kaundika maoni
na maswali yao kujibiwa moja kwa moja,
Alisisitiza
pia kwamba pia mfumo huu unatumika kama promotional tool kwa maana
bidhaa ambazo tunataka ziende duniani kirahisi zinawekwa katika mfumo na
wafanyabiashara wanazipata kirahisi, kupunguza gharama za ufanyaji wa
biashara na kuboresha mazingira ya biashara kwa ujumla.
Mpaka sasa BRELA wameweza kuweka taarifa ya bidhaa 26 za kupeleka nje ya nchi (export) na 13 za kuingiza ndani ya nchi (import)
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) wamesema kwamba wameamua kushiriki kwenye maonyesho ya kilimo ya nane nane yanayoendelea mkoani Simiyu kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko ya nje
Hayo yalisemwa na Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana Senzo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayofanyika mkoani Simiyu.
Alisema wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo hasa ukizingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya nane nane ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja dhima ya kujenga uchumi wa viwanda.
Suzana alisema hivyo vyote vinaenda sambamba na uwezeshaji biashara huku akieleza lengo kubwa la mfumo ni kuhakikisha wakulima na wazalishaji wa bidhaa nchi wanapata taarifa za mahitaji ya masoko ya nje .
“Kwa mfano mtu anataka kusafirisha bidhaa kupeleka Ulaya ,ni rahisi sana kupata taarifa hizi katika mfumo wa trade facilitation information module ambapo hapo awali haikuwepo kabisa”Alisema
Aidha alisema kwa mkoa huo wafugaji wengi hivyo wafugaji ni wengi hivyo ukitaka kujua taarifa zinazohusu vibali na leseni mbalimbali katika kupeleka mifugo yake katika soko la nje ni rahisi kwasababu taarifa zipo ambazo zitamuwezesha kujua nini anahitaji, kwa gharama gani, itachukua muda gani, aendee taasisi gani na iko wapi.
Aliongeza kwamba kwa mantiki hiyo mfumo huu ni mwarobaini wa tatizo la taarifa za kibiashara katika upatikanaji wa vibali na leseni mbalimbali nchini huku wakiwakaribisha wananchi kufika kwenye banda lao kupata huduma hizo.
“Lakini pia BRELA tunatoa leseni za kundi A kama zilivyoainishwa katika sheria Leseni za Biashara ya Mwaka 1972 na marekebisho yake…. Leseni za kundi A ni zipi, ni zile leseni zinazotolewa kwa biashara zenye mlengo wa kitaifa, kimataifa na zenye usimamizi maalum, biashara hizi ni kama usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, uingizaji wa bidhaa ndani ya nchi na biashara za usimamizi maalum kama za madini, benki na zingine kama hizo.
Awali akizungumza Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela suzana Senso amesema wapo kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko ya nje (internatinal market) .
Hivyo bas mkulima / mfanyabiashara akifika BRELA anapata taarifa za kibishara zaidi katika biashara za kimataifa,asajili kampuni au jina la biashara na anapata leseni itakayomuwezesha kusafirisha bidhaa zake nje ya nchi.
Hata hivyo alisemwa kwamba kwa matiki hiyo sasa Brela ni one stop shop mfanyabiashara akifika hapa anapata kila kitu kitakachomuwezesha kwenda kufanya biashara duniani.
Naye kwa upande wake Eliabu Rwabiyago ambaye ni Afisa kutoka Brela amesema wakala pia ina kitengo cha kuwezesha biashara (trade facilitation section) ambacho kimejikita katika uwezeshaji biashara.
Alisema kwa sasa wakala huo unaandaa portal inayoitwa trade facilitation information module , portal ambayo itajikita katika kutoa taarifa za kibiashara nchini.
Alisema kwasababu wafanyabiashara wengi nchini na nje ya nchi wanataka kufanyabiashara lakini taarifa za kibiashara kwa maana ya vibali na leseni mbalimbali zinazohitajika zinapatikanaje na kwa muda gani hivyo kwa mtandao hayo maswali yote yamejibiwa.
Alieleza kwamba kukamilika na kutumika kwa mfumo huu kutakuwa na faida nyingi sana katika uwezeshaji wa biashara ikiwemo kuongeza uwazi katika utoaji wa huduma za umma, kuiongeza ushirikiano baina ya ofisi za umma na wafanyabiashara maana kwa kutumia mfumo watakuwa wanaweza kaundika maoni na maswali yao kujibiwa moja kwa moja,
Alisisitiza pia kwamba pia mfumo huu unatumika kama promotional tool kwa maana bidhaa ambazo tunataka ziende duniani kirahisi zinawekwa katika mfumo na wafanyabiashara wanazipata kirahisi, kupunguza gharama za ufanyaji wa biashara na kuboresha mazingira ya biashara kwa ujumla.
Mpaka sasa BRELA wameweza kuweka taarifa ya bidhaa 26 za kupeleka nje ya nchi (export) na 13 za kuingiza ndani ya nchi (import)
No comments :
Post a Comment