Friday, August 2, 2019

MSIMU WA MAONESHO YA NANENANE 2019, PSSSF YAAHIDI KUTOA HUDUMA BORA NA ZENYE VIWANGO


Mwananchi huyu (watatu kulia), akipatiwa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) alipotembelea banda namba 37 la Mfuko huo kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Simiyu, Bw.Mawazo Ngeraniza (kulia), akitoa elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii kwa wanachama wa PSSSF waliotembeela banda la Mfuko huo kwenye maonesho hayo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Rehema Mkamba akimfafanualia jambo mwanachama wa Mfuko alipotembelea banda la Mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Rehema Mkamba akimfafanualia jambo mwanachama aliyefika kuhudumiwa.
Timu ya PSSSF iliyoweka kambi kwenye banda namba 37 la Mfuko huo mkabala na BoT kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Afisa Mafao Mwandamizi PSSSF, Bi.Linda Balati (kulia), akimweleza mwananchi huyu (kushoto)kuhusu masuala ya hifadhi ya Jamii, alipotembeela banda la Mfuko kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Katikati ni Afisa Matekeelzo PSSSF Mkoa wa Simiyu, Bw. Mohammed Nyengi.
Afisa Matekelezo PSSSF Mkoa wa Simiyu, Bw. Charles Muhoni (kulia), akitayarisha taarifa za michango za Mwnaachama huyu kushoto, aliyetembeela banda la PSSSF viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Afisa Mafao Mwandamizi PSSSF, Bi.Linda Balati (kulia), akimkabidhi mfuko wenye taarifa mbalimbali za PSSSF, mwanachama huyu aliyefika kujua taarifa za michango yake.
Mmoja wa wanachama waliotembela banda la PSSSF akiangalia taarifa za michango yake.
Afisa Mafao Mwandamizi PSSSF, Bi.Linda Balati (kulia), akimfafanualia mwanachama huyu kuhusu hali ya michango yake.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Rehema Mkamba (katikati), akishirikiana na Afsia Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. Charles Muhoni wakati akiandaa taarifa za michango za mwanachama wa Mfuko aliyetembelea banda la Mfuko huo ili kujua hali ya michango yake.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeahidi kutoa huduma bora na za uhakika wakati wa msimu huu wa maonesho ya Nanenane mwaka huu wa 2019 yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu na kwenye Kanda tatu za Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Mashariki.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bi. Rehema Mkamba ameyasema hayo leo Agosti 2, 2019 kwenye viwanja vya Nyakabidni nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

“Tunawahamisha sana wananchi na wanachama wetu kutembelea kwenye mabanda yetu katika maonesho haya yanayofanyika kitaifa hapa Nyakabindi, lakini pia Kikanda, na tuna Kanda ya Kaskazini maonesho yanafanyika jijini Arusha, Kanda ya Mashariki, mkoani Morogoro na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini maonesho yanafanyika jijini Mbeya.” Alifafanua Bi. Mkamba.
“Tunaamini kuwa maonesho ya nanenae hapa Nyakabindi na kwenye Kanda nilizotaja ni jukwaa zuri kwa Mfuko wa PSSSF ambao unahudumia watumishi wa Umma kukutana na wanachama wetu ambao taasisi nyingi za Umma zinashiriki katika maonesho hayo, hivyo nitoe wito kila wapatapo nafasi wapitie kwenye banda letu ili tuwahudumie kama ambavyo wangehudumiwa kwenye ofisi zetu zilizoenea kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.” Alisisitiza.
Katika mabanda yetu tunatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa za Pensheni ya Uzeeni, taarifa za Mafao ya kukosa Ajira, taarifa za Mafao ya Uzazi, taarifa za Dhamana ya Mikopo ya Nyumba, taarifa za Uwekezaji lakini pia wastaafu watapata fursa ya kuhakiki taarifa zao zoezi ambalo ni endelevu.” Alifafanua Bi. Mkamba.
Alisema PSSSF ni Mfuko ulioanzishwa mwaka mmoja uliopita baada ya kuunganishwa kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF.

No comments :

Post a Comment