| Meneja wa Pori la Akiba la Selous, Henock Msocha ( kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati walipotembelea eneo amvalo lilikuwa na mgogoro kati ya Kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous |
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akionesha eneo la
Pori Tengefu akiwa kwenye kigingi ambacho ni mpaka kati ya eneo la
Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya wananchi wa kijiji
cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous ambalo limekuja kubainika
kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji hicho na wala sio sehemu ya Pori la
akiba la Selous bali ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa
kwa ajili ya kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous
katika wilaya Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo
la Liwale, Zuberi Kuchauka
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa
Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka wakiwa kwenye eneo la kigingi huku
Mbunge huyo akiomuonesha Naibu Waziri Kanyasu eneo la Kihurumira ambalo
lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na
Pori la Akiba la Selous ambalo limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio
ardhi ya Kijiji hicho na wala sio sehemu ya Pori la akiba la Selous bali
ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa kwa ajili ya
kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous katika wilaya
Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Liwale,
Zuberi Kuchauka
Baadhi
ya wananchi wakiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu wakiangalia eneo la Kihurumila sehemu ambayo
kuna mto na ambalo lilikuwa na mgogoro kuwa sio mali ya pande zote
mbili bali mali ya serikali kuu inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii,
Mbunge
wa Liwale, Mhe.Zuberi Kuchauka akizungumza na wananchi wake kuhusu
kumalizika kwa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 12 baada ya Naibu
Waziri Kanyasu kuzungumza na wananchi hao
Baadhi
ya wananchi wakiwa wanatoka eneo lenye mgogoro ambapo walitaka eneo
hilo la mto waweze kilitumia kwa ajili ya kulishia mifugo pamoja na
kulima katika mto huo ambapo kutokana na hali hiyo mto huo usingeweza
kudumu kwa muda mrefu
Aniel
Heliem mmoia wa wananchi akimuuliza swali Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Cinstantine Kanyasu mata baada ya kuutangaza kuwa eneo la
Kihurumila si sehemu ya Pori la Akiba la Selous na wala sio eneo la
Kijiji cha Kikulyungu.NA WMU, LINDI
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametatua mgogoro
uliodumu kwa miaka 12 baina ya Pori la Akiba la Selous na Wananchi wa
kijiji cha Kikulyungu kilichopo katika wilaya ya Liwale mkoani Lindi
Mgogoro
huo wa ardhi ulianza mwaka 2007 ambapo wananchi walianza kudai kuwa
eneo la Kihulumira ambalo linapakana na Pori la Akiba la Selous kuwa
ni moja ya maeneo yao ya Asili.
Kufuatia
hali ilipelekea uhasama mara kwa mara kati ya wananchi na askari
wanyamapori hasa pale wananchi walipokuwa wakikamatwa kwa madai kuwa
wameingia ndani ya Hifadhi bila kibali.
Akizungumza
na wananchi wa wa kijiji cha Kikulyungu mara baada ya kutembelea eneo
lililokuwa na mgogoro, Kanyasu alisema eneo hilo lilisajiriwa mwaka
1975 na kijiji kilisajiriwa mwaka 2005 hivyo eneo hilo si sehemu ya
kijiji.
Amesema
baada ya kuundwa timu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na wataalamu wa Ardhi
kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazo ilibainika kuwa
eneo hilo si la wananchi na wala sio sehemu ya Pori la Akiba la
Selous bali ni Pori Tengefu ambalo ni mali ya serikali Kuu na
linasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Katika
hatua nyingine, Kanyasu amewataka wananchi kuacha vitendo vya kukata
miti ovyo na kuchoma misitu kutoka na uharibifu mkubwa wa misitu
aliuona karibu na eneo lililokuwa na mgogoro baina ya pande hizo mbili.
Kufuatia
hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewaagiza viongozi wa vijiji hivyo kuweka
sheria kali ili kudhibiti hali ya uharibifu wa misitu unaoendelea
katika maeneo hayo.
Akizungumza
kwa niaba ya wanachi wa wilaya ya Liwale Mbunge Liwale, Zuberi
Kuchauka ameishukuru serikali kwa hatua iliyofikia kwani mgogoro huo ni
wa muda mrefu na ulikuwa haujapatiwa ufumbuzi
Amesema
mgogoro huo uliwafanya wananchi wa maeneo hayo kupunguza kasi ya
kujiletea maendeleo badala yake wajanja wachache walikuwa wakitumia
nafasi ya mgogoro kuendelea kujinufaisha.
" Sitegemei mgogoro mwingine wa ardhi baada ya kumalizika huu, Nawaomba wananchi sasa tuchape kazi" Alisisitiza Kuchauka.
Kutokana
na kumalizika kwa mgogoro huo wananchi wa kijiji hicho wameiomba
serikali kulitumia eneo hilo kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori
ili kuinua kipato katika kijiji hicho.
No comments :
Post a Comment