Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akimvalisha cheo
Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Merkiory Komba kuwa Mrakibu wa Magereza
katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2019. Mrakibu
wa Magereza, Merkiory Komba ni Msaidizi wa Mkuu wa Jeshi hilo.
![]() |
| Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akimvalisha cheo Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Lipina Lyimo kuwa Kamishina Msaidizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2019. |

Baadhi
ya Maafisa waliopandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali wakiwa timamu
kabla ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike kuwasili
kwa zoezi la uvishaji vyeo , jana Agosti 6, 2019 kwenye viwanja wa Chuo
cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam.

Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akikagua Gwaride
maalum kabla ya zoezi la uvishaji vyeo kwa Maafisa wa Mkoa wa Dr es
Salaam na Mkoa wa Pwani waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni.

Gwaride
maalum likipita kwa mwendo wa pole mbele ya Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini(hayupo pichani) kwenye hafla ya uvishaji vyeo kwa
maafisa wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani jana Agosti 6, 2019.

Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima wakati Gwaride maalum
likipita mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani)
kwenye hafla ya uvishaji vyeo kwa maafisa wa Mkoa wa Dar es Salaam na
Mkoa wa Pwani jana Agosti 6, 2019.

Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maofisa wa ngazi mbalimbali wa Jeshi la Magereza
waliopandishwa vyeo (waliosimama)baada ya hafla uvishaji vyeo
iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga
jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2018(Picha zote na Jeshi la
Magereza).

No comments :
Post a Comment