Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amezindua
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jengo la tatu
(Terminal 3), jijini Dar es salaam mradi ambao unagharimu zaidi ya
Bilioni 720.
Akizumgumza kwenye uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema licha ya Serikali
yake kutekeleza mradi huo, lakini hadhani kama watakaofuata kwenye
nafasi hiyo ya Urais wataweza kuyatimiza anayoyafanya, kwa kile
alichokieleza amekuwa akisemwa mara kwa mara.
“Mara
nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo
tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu
waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa
nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila
palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.
“Siwezi
nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni
dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua
hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya
hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania,
inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.
“Ninamshukuru
Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania
wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa
ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi
ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.
No comments :
Post a Comment