Wednesday, August 21, 2019

GAVANA WA BoT, FLORENS LUOGA AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA (AFRICA GROUP 1) ANNE KABAGAMBE JIJINI DAR ES SALAAM


 GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga, (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika (Africa Group 1), Bi. Anne Kabagambe, alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2019.
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga, (kushoto) na timu yake, akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika (Africa Group 1), Bi. Anne Kabagambe na timu yake ofisni kwa Gavana jijini Dar es Salaam. (PICHA NA INNOCENT MMARI WA BoT). 

NA MWANDISHI WETU.
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga, amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya
Afrika (Africa Group 1), Bi. Anne Kabagambe, ofisini kwake jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2019.
Gavana Luoga amemweleza Bi. Kabagambe hatua mbalimbali ambazo BoT inachukua kuhakikisha kuna ukuaji wa uchumi, kuimarisha sekta ya mabenki, mifumo ya malipo na huduma jumuishi za kifedha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia aliipongeza BoT kwa hatua mbalimbali inazochukua kutekeleza sera ya fedha na kueleza utayari wa Benki ya Dunia kushirikiana katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Katika mazungumzo hayo pia Manaibu Gavana wa BoT, Dkt. Yamungu Kayandabila na Dkt. Bernard Kibesse na Mshauri Mwandamizi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji huyo, Bw. Zarau Kibwe, walihudhuria.

No comments :

Post a Comment