Wednesday, August 21, 2019

ALVARO RODRIGUEZ AAGANA NA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU NA KUIMWAGIA SIFA SERIKALI YA RAIS MAGUFULI



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Agost 21,2019 amekutana na kuzungumza na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez Wakati Bw. Alvaro alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa Nchini




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akutana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa,anaye maliza muda wake hapa Nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez .kwa ajili ya kumuaga Waziri Mkuu ofisini kwake .Magogoni jijini Dar es Salaam.leo Agosti 21.2019

UMOJA wa Mataifa (UN) umeipongeza Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna inavyotumia vizuri rasilimali zake za ndani na hivyo kuiwezesha kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo sambamba na kupunguza utegemezi kutoka nje.

Pongezi hizo zimetolewa leo (Jumatano, Agosti 21, 2019) na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez kwa nyakati tofauti wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam.

Mratibu huyo Mkazi wa Umoja wa Mataifa ambaye alikwenda kuagana na viongozi hao baada ya kumaliza muda wake wa utumishi wa taasisi hiyo ya Kimataifa hapa nchini alisema  Tanzania imeendelea kutumia vizuri mapato yake ya ndani kwa kuimarisha miundombinu na huduma za kijamii kama ujenzi wa hospitali na vituo vya afya.

“Katika kipindi changu cha miaka mitano ambacho nimefanya kazi Tanzania, nimeshuhudia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayofanywa na Serikali, ikiwemo kuimarika kwa mahusiano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa na taasisi zake nchini.”

Katika hatua nyingine, Bw. Rodriguez ameisifu Serikali ya Tanzania kwa namna ilivyoweza kuandaa na kuendesha vizuri mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.

Mbali na kuisifu Serikali pia kiongozi huyo amevipongeza vyombo vya habari kwa jinsi vilivyoshirikiana na Serikali kuripoti matukio mbalimbali ya mkutano huo. “Nawapongeza na wananchi kwa ushirikiano walioutoa kwa Serikali wakati wote wa mkutano wa SADC.”

No comments :

Post a Comment